Elizaberth Msagula,Lindi
 

HATIMAYE,ucheleweshaji  wa Fedha za malipo ya wakulima wanaohudumiwa na chama kikuu cha Ushirika Runali kinachojumuisha wakulima wa Wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea Mkoani Lindi, itabaki historia baada ya chama hicho kujenga vituo vya  malipo kwa wilaya za Ruangwa,Liwale na Nachingwea vitakavyotumika kuandaa na kuhakiki malipo ya wakulima hao kwa haraka zaidi.

Miongoni mwa vituo hivyo ni pamoja na kilichojengwa Wilayani Ruangwa ambacho mapema hii leo juni 4,2024 kabla ya kuanza kwa Jukwaa la maendeleo ya ushirika kimewekewa jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akiwakilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Zuwena Omary na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali Wilayani humo pamoja na viongozi wa vyama vya Msingi, Amcos za Wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale yenyewe.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Chama kikuu cha Ushirika Runali, Jahida Hasani ujenzi huo wa kituo cha malipo umegharimu kiasi cha shilingi Milion 110 na kwamba kitaanza kutumiwa katika msimu huu wa zao la ufuta wa mwaka 2024/2025.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama kikuu hicho Odas Mpunga alieleza kuwa lengo kubwa la kujenga kituo hiko ni kuendelea kuwaweka pamoja viongozi na watendaji wa vyama vya msingi kuchakata na kurahisisha mchakato wa malipo ya wakulima lakini pia wanaendelea na uwekezaji kwa kununua lori aina ya Scania lenye uwezo wa kubeba Tan 20 za mazao ya wakulima kwa pamoja kutoka shambani mpaka kwenye maghala.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Katibu Tawala wa Mkoa huo Zuwena Omary baada ya kukagua jengo hilo na kuweka jiwe la msingi amekipongeza chama hicho kwa namna kinavyoendelea kuwekeza na kutoa huduma bora kwa wananchama wake kwa kuzikabili changamoto wanazokutana nazo.

Pamoja na pongezi hizo  pia aliutaka uongozi wa Bodi wa chama hicho cha Runali kutunza mradi huo na kuutumia kama walivyokusudia na kuendelea kusogeza  huduma hiyo katika maeneo ambayo yanawanachama wao na wakulima wengi zaidi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...