Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi. Doris Mollel, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus, katika Makao Makuu ya Shirika hilo huko Geneva.
Mazungumzo yao yalihusu ushirikiano katika kufikia #AfyaKwaWote na kupunguza vifo vya watoto wachanga barani Afrika na duniani kote.
Katika mazungumzo hayo, Bi. Mollel alielezea jinsi ambavyo Taasisi ya Doris Mollel inafanya kazi nchini Tanzania, hasa katika kuboresha miundombinu ya utoaji huduma kwa watoto wachanga, hasa wale wanaozaliwa kabla ya wakati.
Kwa upande wake, Dr. Tedros aliipongeza Taasisi hiyo kwa juhudi zake katika mapambano hayo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano..jpeg)

Mazungumzo yao yalihusu ushirikiano katika kufikia #AfyaKwaWote na kupunguza vifo vya watoto wachanga barani Afrika na duniani kote.
Katika mazungumzo hayo, Bi. Mollel alielezea jinsi ambavyo Taasisi ya Doris Mollel inafanya kazi nchini Tanzania, hasa katika kuboresha miundombinu ya utoaji huduma kwa watoto wachanga, hasa wale wanaozaliwa kabla ya wakati.
Kwa upande wake, Dr. Tedros aliipongeza Taasisi hiyo kwa juhudi zake katika mapambano hayo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...