Na Mwandishi Wetu


TUME ya Taifa ya Ushindani (FCC) imesema itahakikisha inaendelea kumlinda mlaji nchini hususani bidhaa zinazotoka katika viwanda vya ndani na vile vya nje.
Kauli hiyo imesemwa Juni 5,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio wakati wa hafla maalum ya uitiwaji wa saini mashirikiano kati ya Time hiyo na Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI), katika utendaji wa kuboresha mazingira ya uwekezaji wa viwanda na kudhibiti uzalishaji wa bidhaa bandia.


Uitiwaji saini kwa upande wa FCC umefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Mhandisi Leodgar Tenga .


Mkurugenzi wa FCC Erio baada ya kusaini makubaliano hayo ya ushirikiano, amesisitiza lengo la kusaini makubaliano hayo ni kuhakikisha kila mmoja anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kukuza viwanda na kudhibiti bidhaa bandia.
“Kusainiwa wa makubaliano haya kutawezesha kufikia malengo ya serikali ya Rais Dk.Samia ya kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.Mahusiano haya yatahusu namna bora ya kubadilishana taarifa hususan utekelezaji wa sheria mbili ambazo FCC tunazisimamia ikiwemo ya Ushindani na ya alama au nembo ya bidhaa zinazowahusu wenye viwanda,” amesema.


Amefafanua kwamba katika majukumu ya CTI kupitia sera na dira zao zinaonyesha ambavyo wanalenga kulinda mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini kwa wenye viwanda kufikia matarajio yao na kukuza uchumi wa viwanda.


Pamoja na hayo amesema FCC wanaendelea kulinda na kushabihisha ushindani, hivyo wanahakikisha wanadhibiti vitu ambavyo vinaweza kuathiri wawekezaji hao ikiwemo ukiukaji wa sheria na makubaliano kuhakikisha havifanyiki.


Akielezea kuhusu sheria ya bidhaa bandia amesema, inazuia kupitia mipaka ya nchi na kutozalishwa nchini, ndiyo maana wamesaini makubaliano hayo kuhakikisha wanalinda uzalishaji huo wenye tija katika kukuza ajira, fursa ya uchaguzi wa bidhaa na kukuza uchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye viwanda Nchini (CTI), Mhandisi Leodgar Tenga, ameipongeza FCC kwa kufanikisha kusainiwa kwa makubaliano hayo yanayotokana na ushirikiano mzuri wa Taasisi hizo mbili.
Amesema kufanikiwa kwa makubaliano hayo ni fursa kubwa ya kuhakikisha kuwa mazingira ya uwekezaji wa viwanda yanalindwa na kufikia azma ya serikali ya sekta hiyo kuchochea ukuaji wa uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...