Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewaita wahitimu wa kidato cha sita ambao waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kwa mujibu wa sheria lakini hawajaripoti hadi leo kuripoti mara moja kwenye makambi yaliyopo karibu makazi yao.

Hivi karibuni Mkuu wa JKT Meja Jenerali, Rajabu Mabele alitoa wito kwa wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa lazima (Kwa mujibu wa Sheria) mwaka 2024.

Vijana hao walitakiwa kuripoti katika makambi waliopangiwa wakiwa na vifaa walivyoainishiwa, kuanzia Juni Mosi, 2024 hadi Juni 7, 2024.

Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Brigedia Jenerali Rajabu Mabena ametangazia vijana wote walioitwa katika mafunzo hayo ya lazima lakini hawajaripoti makambini hadi sasa, kuripoti mara moja katika makambi yaliyo karibu na makazi yao.

Brigedia Jenerali Mabena amesema kwa kawaida vijana wanaenda kusoma katika maeneo tofauti nchini, hivyo kutokana na utaratibu wa kuwapangia makambi yaliyo karibu na shule walizosoma wengine wanajikuta wakilazimika kugharamia nauli kubwa kwenda kwenye makambi hayo.

“Lakini unaweza kukuta kijana amekwenda kusoma Songea (Ruvuma) lakini yeye anaishi Musoma (Mara). Na wote tunajua hali za kiuchumi. Tumekuwa tukipata simu nyingi sana kutoka kwa wazazi na baadhi ya walezi wakiomba vijana wao kubadilishiwa makambi,”amesema.

Amesema wengi wa vijana waliopangiwa walishindwa kuripoti kwa kukosa nauli na kwa kuwa walezi na wazazi walionyesha changamoto hiyo wakati walipokuwa wakiwapigia simu, JKT imeamua kuwaruhusu kuripoti katika makambi yaliyo jirani.
 
“Sisi tulizingatia hili ndio maana katika tangazo hili tumewaambia kuwa vijana hawa (wasioripoti hadi sasa), waripoti katika makambi ambayo yako karibu nao (makazi yao),”amesema.

Aidha, Brigedia Jenerali Mabena amesema JKT imetoa nyongeza awamu ya pili ya vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2024, kujiunga na jeshi hilo ili kufanya mafunzo hayo ya lazima.

Amesema orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo awamu ya pili na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni WWW.jkt.go.tz.

Brigedia Jenerali, Mabena amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya jeshi hilo kuanzia Juni 22,2024 (leo) hadi Juni 26,2024.

Vifaa vinavyohitajika kwa vijana kujiunga na mafunzo hayo ni -:

1. Bukta ya rangi ya "Dark Blue) yenye Mpira kiunoni, iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu.

2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)

3. Raba za michezo yenye rangi ya ya kijani Blue

4. Shuka Mbili za kulalia zenye rangi blue bahari.

5. Soksi ndefu za za rangi nyeusi.

6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa Mikoa yenye baridi.

7. Track suit ya rangi ya kijani kwa au blue

8. Nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na Elimu ya juu, zikiwemo vyeti vya kuzaliwa, vyetie vyae kuhitimu kidato cha nne

9. Nauli yae kwenda makambini na kurudi nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...