Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii leo Jumapili 30 Juni 2024 imetembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jijini Dar es Salaam.

Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni mradi wa Morocco Square pamoja na miradi ya Samia Housing Scheme na ule wa 711 iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameongoza ujumbe wa Wizara ya Ardhi pamoja na ule Shirika la Nyumba la Taifa katika ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge iliyoongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mzava.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda ameishukuru kamati ya Bunge kwa ushauri inayoutoa kwa wizara alioueleza kuwa, umeisaidia wizara na taasisi zake kuboresha shughuli zake.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwezesha miradi ya Shirika la Nyunba la Taifa iliyosimama kwa muda mrefu kuendelea.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...