Na Avila Kakingo, Michuzi Tv

KANISA La Pentekoste Tanzania (KLPT), leo Juni 21, 2024 limeongoza ibada kwaajili ya kumuaga na kumpongeza, Mwangalizi Mkuu Mstaafu wa kanisa hilo, Askofu Dkt. Philemon Tibanenason ambaye ametimiza miaka 58 ya uhudumu katika kanisa la Mungu hapa nchini.

Mchungaji Dkt. Philemon Tibanenason alianza kulitumikia kanisa mara tuu baada ya kuoa mwaka 1966 akiwa na Umri wa Miaka 24 ambapo mpaka sasa ana umri wa miaka 82.

Mchungaji Dkt. Tibanenason akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa ibada maalumu amemshukuru Mungu kwa kupewa maua yake (sifa) angali mzima ambapo ni tofauti kwa watu wengine ambao hupewa sifa wakiwa wamefariki dunia.

"Namshukuru Mungu waumini (Kanisa la Mungu) kwa kunisifia ningali mzima na ninaafya na ninaweza kusimama hapa tena na kuzungumza na kanisa la Mungu......"

Askofu Dkt. Tibanenason akizungumza huku akionesha tabasamu mbele ya Madhabahu ya Mungu amesema anawashukuru Kanisa la Mungu pamoja na Mama yake Mzazi aliyemuusia mambo mbalimbali mema hasa 'Kusema Ukweli na kutowadanganya watu'.

Akizungumza huku akitolea mifano mbalimbali pamoja na kuongoza kuimba nyimbo anazozipenda Askofu Dkt. Tibanenason amesema kuwa kazi yake imeisha.

" Sio kama nitaondoka kesho lakini hata kama nikiendelea kuishi, wewe ambaye umeniona leo utakuwa na kumbukumbu ... Nimeyasikia mambo ambayo walikuwa wanayasema juu yangu ni wachache wanaosikia maneno ambayo mlikuwa mkisema juu yangu, nashukuru mmesema kitu kizuri ambacho nimekiona..." Ameeleza Askofu Dkt. Tibanenason

Amesema kuwa amefika si kwa sababu amepanga kufika lakini Mungu amepanga afike, Mungu hawapi wanadamu wakati kama bidhaa ya kujitajilisha bali ametoa wakati ili wanadamu wautumie kwa kumsifu Mungu, kwa Kumtumikia Mungu na pia katika wakati huo waweze kuishi kwa kusudi alilowavuvia la kutunza wakati.

Amesema wakati ni bidhaa ambayo ukiipoteza kweli unakuwa umeisha, ukiupoteza wakati utaujutia na haiwezekani kuurudisha nyuma. Ni kweli unaweza kuomba msamaha Mungu akakusamehe lakini sio muda.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ibada ya kumuaga Mwangalizi Mstaafu huyo kuhusiana na maadili ya Kitanzania, Mwangalizi wa Kanisa la KPLT Rev. Dkt Fanuel Shekihiyo amesema kuwa kwasasa lazima kupambana na maadili ya kila familia.

" Kwanza tutaanza kuimarisha mafundisho ya ndoa na mafundisho ya jamii kwa ujumla na kufundisha neno la Mungu la kweli litakalowafanya watu wa Mungu kuwa na matendo mema na kuacha matendo mabaya."

Amesema kanisa la KLPT linaungana na serikali kukemea matendo maovu yanayotendeka katika jamii.

"Kama Kanisa tutaungana kwa pamoja kama mwili wakristo kwa maombi kwa mafundisho na kuzungukia maeneo kwa ajili ya kutoa elimu ili jamii nzima iweze kubadilika na kuwa na jamii yenya maadili. "

Kwa Upande wa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Malasusa amempongeza Askofu Dkt. Tibanenason kwa kutimiza miaka 58 ya utumishi wake katika kulitumikia kanisa kwa uadilifu mkubwa na kwa nguvu zake.

Pia amesema amemfahamu Askofu Dkt. Tibanenason kwa sababu alikuwa anatumika mahala popote ambapo Mungu alikuwa akimchagua kutumika, pia amekuwa kiunganishi kati ya Kanisa na watu katika utumishi wake wakati alipokuwa Mwenyekiti wa makanisa jijini Dar es Salaam kwa kipindi kirefu.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...