Na Fauzia Mussa, 27/06/2024

Utowaji wa talaka kiholela kwa wanandoa imetajwa ni moja ya jambo linalochangia kwa asilimia kubwa kukithiri mporomoko wa maadili na kushamiri kwa vitendo vya udhalilishaji kwa watoto.


Mwenyekiti wa baraza la wawakilishi Mhe. Mwanaasha Khamis Juma ameyasema hayo wakati akifunguwa kongamano la malezi kwa jamii ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za wiki ya msaada wa kisheria.


Amesema watoto wengi hukosa maadili kutokana kukosa usimamizi mzuri wa malezi ya baba na mama mara baada ya wao kuachana.


Amefahamisha kuwa wazazi wanamchango mkubwa katika kuinyoosha jamii kimaadili hivyo kitendo cha baadhi ya wanandoa kutengana kunawakosesha fursa watoto ya kupata malezi bora kutokana na kukosa ukaribu na wazazi wao.


Amesema kongamano hilo litasaidia kuielimisha jamii kufahamu namna bora ya kuzilea ndoa zao na kuimarisha malezi bora kwa watoto.

Aidha Mhe. Mwanasha amesema msaada wa kisheria imekuwa mkombozi mkubwa kwa wanajamii waliokata tamaa ya kupata haki zao kwani imesaidia kuondosha migogoro mbalimbali inayowakabili wanajamii ikiwemo migogoro ya kindoa na migogoro ya ardhi.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Raisi, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora anayeshuhulikia masuala ya katiba na sheria Mzee Ali Haji na Mkurugenzi Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma kutoka Tanzania Bara wamesema maadili hayajengwi na sheria hivyo ni vyema kwa wazazi kubadilika kwa kukilea kizazi katika maadili mema yanayoenda samabamba na mila, silka na utamaduni wa mtanzania.


Wakitoa mada katika kongamano hilo baadhi ya Mashekh walioshiriki mkutano huo wamesema jukumu la kurekebisha jamii katika melezi tayari limewekewa miongozo thabiti katika vitabu vya dini hivyo si vyema kwa wanajamii kwemda kinyume na mafundisho hayo ili kupata kizazi kilicho bora.


Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamewalalamikia baadhi ya wanaume kuwatekeleza watoto wao na kuwaachia jukumu la ulezi wanawake peke yao.

Wiki ya msaada wa kisheria hufikia kilele chake juni 28 ikiwa na kauli mbiu "Tumia teknolojia kurahisisha upatikanaji wa haki".



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...