NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa aliyekuwa Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro marehemu Tixon Nzunda alikuwa kiongozi wa umma mwadilifu katika kuwatumikia wananchi na kila mara alikuwa na hofu ya kuwatanguliza wananchi.

Mapango alitoa kauli hiyo leo alipofika nyumbani kwa marehemu kusaini kitabu cha maombolezo pamoja na kuifariji familia na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro ambapo alisema kuwa, marehemu Nzunda ameacha mfano wa kuigwa na watumishi wa umma.

Alisema kuwa, yeye anamkumbuka vizuri marehemu kwani alipokuwa Waziri wa Fedha alikuwa anakaa nae sana marehemu akiwa ofisi ya Waziri Mkuu kwenye vikao vyao vya utatu na wafanyakazi ambapo alikuwa mtu makini sana na mpole.

“Kwa upande wa Serikali tukio hili limetuumiza sana kwa niaba ya Serikali na mimi mwenyewe na Rais yupo safarini tunasema poleni sana na niwashukuru kwa moyo wenu toka tukio hili litokee mmekuwa pamoja na familia huu ndio Utanzania ninaoufaham” alisema Makamu wa Rais Dkt. Mpango.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akitoa ratiba ya mazishi   alisema July  21 saa 4:00asubui mwili wa marehemu  Dk Tixon Nzunda  utafikishwa nyumbani kwake na kufanyiwa ibada fupi ambapo  wananchi wa mkoa wa kilimanjaro watapata fursa ya kuaga.

"Saa 10:00 jioni  msafara huo utaanza safari ya kuelekea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam (Goba) kupitia ufanya wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)  kwa ndege aliyotoa  serikali.Mwili utalala nyumbani hapo ukimsubiria mtoto wake aliyepo nchini India anayetarajiwa kufika ijumaa  saa tatu.

Siku hiyo, wananchi wa Dar es Salaam  wakiwemo na majirani watapata fursa za kuaga mwili, na kisha mwili utapelekwa uwanja wa  ndege wa mwalimu Julias Nyerere kwa ajili ya kwenda kijijini kwao  mkoani Songwe kwa ajili ya maziko yatakayofanyika jumamosi July 22 mwaka huu,"alisema Babu 

Alisema pamoja na hilo,  mwili  dereva wake Alphonce Edson (54) unatarajiwa kuzikwa July 24 nyumbani kwake  Mabogini Chekereni.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...