Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Imeelezwa kuwa uamuzi wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza maboresho ya huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania ndani ya miaka mitatu umeongeza ufanisi katika maeneo mbalimbali kama vile,Miundombinu, eneo la Tehama na Ongezeko la Watumishi.

Hayo yameelezwa mapema leo hii Juni 5,2024 Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel katika mkutano wake na Wanahabari wakati akielezea mafanikio ya miaka ya Dkt Samia katika Mahakama kwa Mkoa wa Dodoma,Taifa na hata Ushirikiano wa Kimataifa ambao Raisi ameendelea kuusimamia vema.

Na kuongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imetoa msukumo wa pekee katika kuiwezesha Mahakama kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kusogeza huduma karibu na Wananchi.

"Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendeleza uboreshaji wa huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania ndani ya miaka mitatu umeongeza ufanisi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo;Miundombinu ya majengo, Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Ongezeko la Watumishi"

"Serikali ya Awamu ya Sita imetoa msukumo wa pekee katika kuiwezesha Mahakama kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kusogeza huduma karibu na wananchi. Miezi michache baada ya kuingia madarakani, Rais aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha majengo ya Mahakama, na kuhakikisha kuwa kila Mkoa unakuwa na jengo la kisasa la Mahakama Kuu".

Aidha Prof. Ole Gabriel amesema katika hicho hicho cha miaka mitatu ya Dkt Samia Serikali imepitisha ajira mpya 762 kwa Watumishi wapya wakiwemo Mahakimu Wakazi 78 na watumishi wasio Mahakimu 684, kufanikiwa kutoa mafunzo kwa Watumishi na Wadau wa Mahakama 8,701 na pia Serikali kuiwezesha Mahakama katika ununuzi jumla ya magari 187 yaliyokwenda kwa Majaji,Naibu Wajasili, Wakurugenzi, Usafiri wa Watumishi na mengine kuelekezwa katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama hapa Nchini.

" Katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali imepitisha jumla ya ajira mpya 762 kwa Watumishi wapya wakiwemo Mahakimu Wakazi 78 na Watumishi wasio Mahakimu 684".

"Katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia, Mahakama ya Tanzania imefanikiwa kutoa Mafunzo kwa jumla ya Watumishi na Wadau wa Mahakama 8,701, Watumishi walionufaika na Mafunzo hayo ni pamoja na Majaji, Mahakimu pamoja na Watumishi wasio Mahakimu".

"Katika kipindi cha miaka mitatu (3) Mahakama ya Tanzania kupitia Serikali imewezeshwa kununua jumla ya magari 187 ambayo yaligawanywa kwa Majaji, Naibu Wajasili, Wakurugenzi, Usafiri wa Watumishi na mengine yalielekezwa kwa ajili ya usimamizi wa Miradi mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama nchini".

Pia ameongelea eneo la matumizi ya Tehama ikiwemo Mfumo mpya wa Usajili,Uendeshaji na Usimamizi wa Mashauri(e-CMS) ambayo amesema kuwa imerahisisha utiaji wa haki kwa Wananchi.

"Matumizi ya mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika Mahakama yamerahisisha utoaji haki kwa Wananchi. Mfumo mpya wa Usajili, Uendeshaji na Usimamizi wa Mashauri (e-CMS) Mfumo wa Unukuzi na Tafsiri ya Mienendo ya Mashauri Mahakamani (TTS) umeboresha utendaji kazi wa Mahakama".

Mwisho ameahidi kuendelea kutoa Elimu Wananchi kwani kumekuwa na changamoto ya uelewa juu ya namna ya Utendaji kazi wa Mhimili wa Mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...