MRADI wa Beginit unaojihusisha na kutoa mafunzo ya Uongozi kwa Watoto Leo Juni 25,2024 umetoa mafunzo ya uongozi kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Temeke na Toangoma wenye lengo la kuwajengea uwezo wa kutafuta fursa katika jamii na kutatua changamoto zilizopo na zabaadae.

Hayo ameyasemwa na Elen Tropinova,ambaye ni Mkuu wa Mradi huo wa Beginit kwenye mafunzo hayo yaliyofanyika Temeke Jijini Dar es salaam.

Aidha,Tropinova ameongezea kwa kusema kuwa mradi huo umefanyika kwa miaka tatu tanzania na hapo mwanzoni walijikita katika mafunzo ya tehama na baadae wakawafundisha ujuzi wa uongozi namna ya kuendesha miradi ya kijamii .

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Indrive Abdul Mwanja amesema faida wanazopata kwenye kampuni hiyo wanarudisha kwa jamii na imerudisha kwa kuwawezesha vijana wadogo kwenye njia tofauti

Nao wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo Meura Moses na kutoka shule ya sekondari Temeke amesema mradi huo umewapa ujasiri na uwezo kwa kuongea mbele za watu juu ya maendeleo ya jamii.
 

Mwanzilishi wa Mradi wa Beginit  Elen Tropinova akizungumza na Wanahabari Leo Juni 25,2024 mara baada ya kuzindua mradi huo wenye lengo la kuwawezesha watoto wakitanzania kujiandaa kuitumikia vyema nchi yao
 

Mnufaika wa Mafunzo ya uongozi kutoka Mradi wa Beginit kutoka Shule ya Sekondari Temeke Meura Moses Leo Juni 25,2024 Temeke Jijini Dar es Salaam akifafanua zaidi namna alivyofaidika na Mafunzo hayo
 

Mwakilishi wa Kampuni ya Indrive ambao ni wadhamini wa Mradi wa Beginit Abdul Mwanja akiongea machache Leo Juni 25,2024 Kuhusiana na Kampuni yao kujitoa kutoa mchango wao Kuhakikisha mafunzo hayo yanafanyika nchini Tanzania kwa Ufanisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...