Mwandishi Wetu,Dodoma

Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kupitia Programa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) limeyataka makundi ya kinamama, vijana na makundi maalumu kujenga nidhamu ya fedha ili kujenga uwezo wa biashara zao kukua na kushiriki katika uchumia wa taifa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Bi. Beng’i Issa wakati baraza hilo lilipoifikisha program ya SIMASA katika mkoa wa Dodoma kuwa makundi hayo yanatakiwa kujenga nidhamu ya fedha katika biashara zao ili ziweze kukua na kusaidia familia zao pamoja na kushiriki katika uchumi wa taifa lao.

“Tunahitaji mjenge nidhamu ya fedha katika biashara zenu ili zikue na kuondokana na vipato duni,” na aliongeza kusema hiyo itasaidia kukuza mitaji na vipato na familia zao kustawi.

Alifafanua zaidi Bi. Bengi alisema nidhamu ya fedha na kuweka akiba inatokana na faida inayopatikana katika biashara hujenga uwezo kwa mfanyabiashara au mjasirimali kupiga hatua.

“Kuweka akiba katika akaunti benki ni usalama wa fedha na siyo kuweka katika kibubu zinaweza kuibiwa na kusababisha hasara,” na kuweka fedha benki ni moja ya kupata fursa ya kukopesheka kukuza mtaji, alisisitiza.

Pia alisema makundi hayo yanahitajika kuwa na malengo ya muda mrefu na munda mfupi ya biashara sababu biashara inahitaji malengo na kuweka mkakati namna ya kutekeleza malengo na kuwekeza zaidi ili fedha iweze kuzaa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi.Rosemary Senyamule alisema mkoa wake umeipokea program ya IMASA na malengo yake na watahakikisha kupitia madawati ya wilaya na mikoa ya baraza wanayafikishia makundi hayo elimu ili yashiriki katika shughuli za biashara na ujasirimali.

“Ninawahitaji wachangamkie fursa zilizopo mkoani kwetu kwa kuanzisha shughuli za biashara na ujasiriamali, na mwaka huu sherehe ya nanenane kitafa zitafanyika kwetu tumieni fursa hii,” hapa tutajifunza na kufanya biashara, alieleza.

Alisema wakulima watapata fursa ya kuuza mazao, chakula na biashara mbalimbali kwa vile watu kutoka mikoa mbalimbali watashiriki na hapo wataweza kujifunza shughuli kama za kilimo, ufugaji, uvuvi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Dodoma mjini, Mhandishi Joha Mtamba alisema wafanyabiashara na wajasirimali watajikomboa kupitia uwezeshaji kutoka program ya IMASA na wamejipanga kuitumia kwa malengo.

“Mkowa mzima tupo hapa na tunataka mabadiliko ya kiuchumi,” na aliongeza kusema wanawake wataitumia IMASA kwa kuwa malengo yake ni kuyainua makundi hayo.

Naye Zainabu Harabu kutoka kata ya Majengo mfanyabiashara wa mbogamboga alisema kupitia programa hiyo aliweza kujifunza namna mabenki yanavyotoa mikopo midogo na mikubwa na namna ya kupata bima ya afya.

“Hii inatuwezesha wajasiriamali kupata fursa ya kushiriki katika biashara sababu ya uwepo wa mikopo mido,”.

Baraza hilo kupitia program ya IMASA linatoa elimu ya uwezeshaji likiambatana na taasisi ya kifedha kama NMB na CRDB ili kuwawezesha wananchi kuimarisha shughuli za biashara na ujairimali.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...