NA WILLIUM PAUL, HAI.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda amefariki Dunia katika ajali ambayo imetokea eneo la Njia panda ya KIA, Wilaya ya Hai, akiwa kwenye ziara Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo na kwamba ajali hiyo imetokea muda wa saa 8 kuelekea saa 9 mchana leo, Juni 18, 2024.

"Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,"amesema RC Babu

Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Katika ajali hiyo inadaiwa kuwa, dereva wake naye kafariki duniani.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...