Na Mwandishi Wetu
CHUO Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeingia katika makubaliano mapya na Kampuni ya Simba Supply Chain Solutions Ltd kwa awamu ya pili ambayo itakuwa ya muda wa miaka mitatu (3) baada ya kumalizika makubaliano ya kwanza ambayo yalifanyika mwaka 2021.
Makubaliano haya yanalenga ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo tafiti, mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi na mafunzo ya uwezeshaji kwa watendaji wa taasisi zote mbili.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam baada ya kutiliana saini, Mkuu wa NIT, Dk Prosper Mgaya alisema MoU itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake pia kuruhusu wanafunzi na wahadhiri wa chuo hicho kufanya attachment katika SSCS.
Aliongeza: “Baada ya miaka mitatu ya MoU na Simba Supply Chain Solution, leo, tumefufua tena ushirikiano wetu ambao utaendelea kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa NIT na hivyo kuwawezesha kuhitimu kama wataalamu wenye uwezo tayari kutumikia soko.
Pia ilieleza kuwa wataalamu wa Simba Supply Chain Solution nao watashirikishwa katika programu za mafunzo zinazoendeshwa na NIT.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kampuni ya SSCS Ajuaye Msese amesema kuwa ushirikiano huu unalenga kuziba pengo la ujuzi katika mtiririko mzima wa thamani katika sekta ya usafirishaji na kutengeneza msingi wa maendeleo ya wafanyakazi ili kufikia uboreshaji endelevu, kuongeza tija na ufanisi katika kazi na mifumo na baadae kuongeza vipato vya taasisi zetu na nchi kwa ujumla.
Msese ameonezea kuwa SSCS imekuwa na uhusiano wa muda mrefu sasa na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa na ambapo wameweza kunufaika kwa kiwango kikubwa kwa mazao mbalimbali yanayozalishwa na Chuo katika kupata waajiriwa wenye sifa lakini pia kupata mafunzo mbalimbali kwa watendaji wetu katika ngazi mbalimbali.
Kwa dhati kabisa, Kampuni yetu ya Simba Supply Chain Solutions Ltd inapenda kukipongeza Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kutokana na namna ambavyo kimekuwa kikishiriki katika kuzalisha wataalam katika kada mbalimbali hususani katika kipindi hiki ambacho nchi imejikita katika kuendeleza viwanda, kufungua fursa mbalimbali na kujenga uchumu imara.
Alisisitiza kuwa Kampuni ya Simba Supply Chain Solutions Ltd ni Kampuni mama inayoongoza Makampuni mengine mawili (Makampuni Dada) ambayo ni Simba Logistics Ltd na Simba Terminals. Kampuni yetu inajishughulisha na usafirishaji kwa njia ya barabara huku ikikita mizizi yake katika huduma za uwakala wa meli, utoaji wa mizigo bandarini, ushushaji na upakiaji wa mizigo bandarini pamoja na utunzaji wa mizigo katika maghala kupitia tawi lake la Simba Terminals. Kampuni yetu imeajiri zaidi ya wafanyakazi 500 huku asilimia zaidi ya 50 ikiwa ni Madereva.
Kutokana na unasaba huo, baina yetu na na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), leo Kampuni yetu ya Simba Supply Chain Solutions Ltd inakwenda kutia saini makubaliano ya ushirikiano na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Kampuni ya Simba Supply Chain Solutions Ltd itaendelea kuwekeza katika nyanja mbalimbali na kutoa fursa kwa watanzania wote, alisema.
Mkuu wa NIT Dk Prosper Mgaya (kulia) akibadilishana hati na Meneja Mkuu wa SSCS, Ajuaye Msese (Kushoto) baada ya kusainiwa kwa Mkataba ambao utaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake pia kuruhusu wanafunzi na wahadhiri kutoka chuo hicho kufanya viambatanisho katika SSCS.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...