Na  Janeth Raphael MichuziTv - Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa suala la matumizi mabaya ya Mamlaka linapaswa kuwa ni jambo la kihistoria hapa Nchini kwa wenye Mamlaka kuzingatia Sheria,Kanuni na Taratibu za Mamlaka hayo.

Dkt Samia amesema hayo mapema Leo hii Juni 15,2024,Jijini Dodoma katika hafla ya kupokea Ripoti ya Kamati ya kuandaa Mkakati wa utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya kuangalia jinai Nchini iliyofanyika Ikulu-Chamwino.

Na kuendelea kuwataka viongozi katika ngazi zote kuendelea kusimamia haki za raia kama zilivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa chachu ya mabadiliko chanya kifikra na kimtazamo.

"Suala la nne ni matumizi mabaya ya madaraka ambayo inatakiwa kuwa jambo la kistoria, Waraka namba moja wa mwaka 2023 wa Katibu Mkuu Kiongozi kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya unaelekeza uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utekelezaji wa Mamlaka yao ya ukamataji, uende ukatekelezwe vyema".

"lakini pamoja na waraka ule ambao umetolewa mapema mwaka jana bado kuna wakuu wa mikoa na Wilaya wanaendeleza ubabe kwenye maeneo waliko. Nasema waraka ule uzingatiwe na uende ukafanye kazi vizuri,kila nafasi ina mipaka yake kwahiyo twendeni kwa mipaka yetu".

Sambamba na hayo pia Dkt Samia wataendelea kufuatilia na kuvipa nguvu vikosi kazi ambao kazi zao bado zinaendelea kwani bado wanasubiri wamalize wapate mapendekezo ili kuendelea na utekelezaji.

"Niseme kwamba tutaendelea kufuatilia na kuzipa nguvu au kuvipa nguvu vikosi kazi ambao kazi zao bado zinaendelea,tunasubiri kwa hamu wamalize tupate mapendekezo yao ili tuendelee na utekelezaji, kwasababu bado wanaendelea basi katibu Mkuu Kiongozi utaendelea kuwapa nguvu kuwapa nguvu na kuwawezesha kuona kwamba kazi hizo bado zinaendelea".

Awali akisoma Taarifa ya Kamati ya Haki Jinai makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa kamati ilianza kazi kwa kuchambua kwa kina ripoti ya Tume na kubaini mapendekezo yalikuwa 333 na kuyagawa katika makundi matatu yaani yani mapendekezo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.

"Mhe Raisi kamati ilianza kazi kwa kuchambua kwa kina ripoti ya Tume na kubaini kuwa ilikuwa na mapendekezo 333,hivyo kamati kwa kushirikiana na Taasisi za Haki jinai iliyagawa mapendekezo hayo katika makundi matatu ambapo mapendekezo 289 yalikuwa ni ya muda mfupi,mapendekezo 37 yalikuwa ni ya muda wa kati na mapendekezo 7 yalikuwa ni ya muda mrefu".

Tume iliundwa January 2023,na kufanyakazi nzuri ambapo 15 July 2023 iliwasilisha taarifa ya kazi yake iliyokuja namapendekezo mbalimbali 333.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2024 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Balozi Ombeni Sefue. Hafla ya upokeaji wa Taarifa hiyo imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kupokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Viongozi wengine kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2024

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...