Raisa Said,Bumbuli.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilida Buriani amewapongeza Halmashauri ya Wilaya Bumbuli, mkoani Tanga kwa  kufikia asilimia 93.5 ya makusanyo ya mapato hali ambayo inaifanya Halmashauri hiyo kuondokana na kuwa ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato kati ya Halmashauri 11 za mkoa huo.

Halmashauri hiyo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka mitatu imekusanya kiasi cha Sh Bilioni 1. 049 hadi kufika Juni 15, mwaka huu kati ya lengo la kukusanya Sh bilioni 1.12 mwaka huu wa fedha 2023/2024. Ukusanyaji umeifanya Halmashauri hiyo kushika nafasi ya tano ya ukusanyaji kati ya Halmashuri 11 za mkoa huo.

Mkuu huyo alisema kuwa hayo ni mafanikio makubwa ambayo wameyapata katika Halmashauri ambayo hapo miaka ya nyuma ilikuwa haifikii malengo ya ukusanyaji ambayo wamejiwekea. “Kuna wakati walikuwa wanakusanya Sh milioni 300,” alisema Dk Buriani. Mkuu huyo wa Mkoa pia ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za serikali (CAG)

Akizungumza katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mkaguzi wa Serikali (CAG)  alisema kuwa ilifikia wakati wakiwa katika mikutano ya TAMISEMI walikuwa wanafikia hatua ya kufikiria kufuta baadhi ya Halmashauri, ikiwemo Bumbuli, ambazo zilikuwa zinashindwa kukusanya mapato na kushindwa kuchangia katika miradi ya maendeleo kama inavyoelekezwa.

Alimpongeza Mwenyekiti wa Halmashauri, hiyo, Amiri Shehiza, madiwani na uongozi mzima wa Halmashauri kwa kazi ambayo wameifanya na kuiondoa Bumbuli katika orodha na aibu ya kuwa ya mwisho kwa ukusanyaji mapato kila mwaka.

 “Kipekee nampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,  Baraka Zikatimu ambaye aliona hali na alichukua hatua mara moja kuhakikisha Halmshauri inaondokan na hali hiyo,” alieleza Dk Buriani ambaye alisema anafahamu utendaji wa  Zikatimu tangu alipokuwa  katika  Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, Mkoani Tabora.

Alisema kuwa Mkurugenzi huyo  ni kijana ambaye anapenda kazi na anapenda kufanya kazi kwa ushirikiano  mbali ya kuwa mtu ambaye anataka umoja.

Aliutaka Mkoa wa Tanga kupunguza hoja 55 za miaka ya nyuma kati ya hoja 71 ambazo bado hazijafanyiwa kazi. Pia amewataka madiwani kwenda katika maeneo ya ukusanyaji mapato kwa siku moja kama mfano na kukusanya mapato.

“Hapo mtaweza kuona ukweli wa ukusanyaji unaofanywa na watendaji wa halmashauri. Kama ukiusanya zaidi ujue ulikuwa unapigwa,” alisema.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Baraka Zikatimu alisema ukusanyaji mapato umekuwa ukipanda kuanzia mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Halmashauri ilikusanya Sh Milioni 559.1 ikiwa ni aslimia 58 ya lengo.

Alisema kuwa ukusanyaji ulipanda mwaka uliofuata mwaka wa fedha 2022/23 ambapo Halmashauri ilikusanya jumla ya Sh milioni 874.1 ikiwa ni asilimia 81

Alizungumza sababu ya kupanda kwa mapato kuwa ni kuziba mianya ya uvujaji wa mapato kwa sababu vyanzo ni vile vile.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,  Pili Mnyema amesema kuwa Halmashauri hiyo ilikuwa inashindwa kutoa asilimia 40 ya mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa muda wa miaka mitatu na akaeleza kuwa juhudi zinazofanywa hivi sasa zitaikwamua halmashauri kutoka katika kadhia hiyo.

alisemakuwa wakati Rais Dk Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani Halmashauri hiyo ilikuwa inakusanya  asilimia 50 ya mapato na akaeleza kuwa viongozi na watendaji hawakukata tamaa hata walipokuwa  kuwa wanapigiwa kelele katika vikao.  

"Walijipanga na kuamua kufanya kazi kwa juhudi na kufikia malengo. Nadhani watendaji wenzangu sasa sitapata barua za kuomba kuhama kutoka Bumbuli kwa sababu hata zile stahiki zenu mlizokuwa mnakosa mtazipata kutokana na kukusanya mapato  kiasi kikubwa," alisema.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri, Amiri Aheziza naliwawpongeza madiwani na watendaji wa Halmashuri kwa juhudi hizo na amesema kuwa makusanyo hayo yataondoa hali ya kuzomewa waliyokuwa wanaipata kila wakifika katika vikao ya kuwa wa mwisho katika ukusayaji wa mapato.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...