Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepongezwa kwa kuendeleza jitihada mbalimbali za kuboresha miundombinu katika sekta ya Utalii nchini ambapo kwa sasa kupitia mradi wa REGROW inatekeleza ujenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI Kihesa Kilolo kitakachosaidia hifadhi za Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.

Mhandisi Mshauri na Meneja wa Mradi huo wa ujenzi wa kituo hicho cha TAWIRI Wilfred Saitoria amebainisha kuwa juhudi anazozifanya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan zinapaswa kuendelezwa na wao kama watekelezaji wanamuunga mkono Mhe. Rais kwa kuhakikisha wanatekeleza ujenzi huo kwa weledi ambapo mradi huo mpaka kukamilika kwake utagharimu zaidi ya Bilioni moja.

“Mradi huu wa ujenzi wa kituo cha utafiti wa Wanyamapori chini ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kilichopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ni juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ulianza mwezi wa pili na unategemea kuchukua miezi 10, utaisha Februari 2025 ulianza mwezi Aprili, ambapo utakapokamilika utaongeza chachu katika sekta ya Utalii”-Alieleza Mhandisi Saitoria.

Baadhi ya Wanufaika waliopata ajira katika mradi huo wakiwemo wanawake kwa wanaume ambao ni vijana wameishukuru serikali kwa kuwafikishia mradi huo ambao umeweza kuwasaidia kupata fedha za kujikimu na kuendesha familia.

“Mimi kama mkazi wa Kihesa Kilolo, huu mradi umetunufaisha sana sisi wenyeji kwa kupata ajira wanakwake kwa wnaume, ajira ambazo tumekutana nazo humu ni vibarua ambapo tunapopata fedha za kujikimu na kuweza kuendesha familia zetu”-Amebainisha Florah Mng’ong’o.

Ujenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Kihesa Kilolo kinachotekelezwa na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania mpaka kukamilika kwake utagharimu zaidi ya Bilioni moja na umetoa ajira kwa Watanzania 30, asilimia kubwa ya wafanyakazi wakiwa ni wazawa wanaotokea maeneo jirani na unapotekelezwa mradi huo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...