NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

SERIKALI imeendelea kuwathamini watu wenye ulemavu nchini ambapo imeendelea kuwapa ajira watu hao huku takwimu zikionyesha toka mwaka 2022 mpaka sasa jumla ya watu wenye ulemavu 1098 wameweza kuajiriwa.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Balozi Emmanuel Nchimbi wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa, alipoingia serikalini walitengeneza utaratibu wa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata ajira ambapo matokeo yake yanaoneka sasa ambapo watu hao wameweza kupata fursa za ajira.

Alisema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kundi la watu wenye ulemavu ambapo fedha hizo wamekuwa wakikopeshwa bila riba na kujinufaisha kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa, kundi hilo pia waliweza kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ambapo kwa sasa serikali inatambua idadi ya watu hao.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo alisema kuwa, kazi kubwa imefanywa na Chama cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwaomba wananchi wa Moshi kuendelea kukiamini Chama hicho pamoja na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la kudumu la wapiga kura na kuwachagua wagombea wanaotokana na CCM.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...