Na Said Mwishehe, Michuzi TV
HEIFER International nchini Tanzania imezindua shindano la AYuTe Africa Challenge kwa mwaka 2024 litakalotoa nafasi kwa vijana wavumbuzi kupata ufadhili na utambuzi wa kukuza mawazo na matarajio yao kwenye sekta ya kilimo.
Lengo la shindano hilo ni kubadilisha mazingira ya kilimo, kukuza uvumbuzi kutoka kwa vijana wa Kiafrika na kufanya kilimo kiwe kazi inayopendeza huku wafumbuzi hao watapewa mitaji na mafunzo ili kutafsiri jitihada na mawazo yao kuwa msaada kwa wakulima wadogo kote nchini.
Akizungumza leo Juni 26,2024 katika ofisi za za Sahara Ventures zilizopo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkazi wa Heifer Tanzania Marck Tsoxo amesema wanatambua nafasi ya Vijana katika teknolojia na uvumbuzi hivyo kupitia Shindano hilo wanaamini watapata wavumbuzi mbalimbali kwa ajilli ya kuendeleza sekta ya Kilimo nchini.
Amesema vijana wako wengi zaidi na asilimia 25 ni watu ambao wanaanzia miaka 35 kwenda juu,lakini kilimo kinahitaji nguvu kazi na hasa ya Vijana huku akifafanua kuwa kwa idadi ya watu,teknolojia na rasilimali zilizopo zinaweza kuleta matokeo makubwa katika sekta ya kilimo.
"Kwahiyo pamoja na umuhimu wa wazee katika kilimo , lakini bado vijana zaidi wanahitajika kwasababu idadi yao ni kubwa.Ukiwapata wengi katika sekta ya kilimo tunaweza kufanya mageuzi makubwa,lakini kwa hulka yao na kwa jinsi walivyolelewa sasa ni watu ambao wanapenda teknolojia.
"Kwa hiyo teknolojia ni muhimu katika katika sekta ya uzalizalishaji wa mifugo na ukweli ni kwamba wakiwepo vijana kutakuwa na uhuishwaji mkubwa wa teknolojia katika sekta ya kilimo.Hivyo mabadiliko yatakuwa makubwa kwa haraka zaidi."
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sahara Venture Jumanne Mtambalike amesema kwa kushirikiana na Heifer wanaweza kuangalia namna gani ya kusaidia vijana hasa wa kitanzania ambao wanafanya shughuli zao za kilimo kwa ubunifu na kupitia teknolojia kutawezesha hizo bunifu zao sokoni kufika katika soko na kutengeneza ajira
"Asilimia zaidi ya 65 ya ajira zinazotoka Afrika ziko katika sekta ya kilimo lakini sekta ya kilimo imechangia asilimia 32 ya GDP katika bara Afrika.Kwa hiyo kwa Kushirikiana na Heifer tunaamini kazi tunayofanya ni muhimu sana katika kuwakwamua vijana na kutengeneza hizo fursa."
Awali Meneja wa Miradi AYuTe Tanzania
Emmanuel Senzige amesema mshindi wa kwanza katika shindano hilo atapatiwa mtaji wa Sh.milioni 28,mshindi wa pili mtaji wa Sh.milioni 21 na mshindi wa tatu atapewa mtaji wa Sh. milioni 14.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...