Kaimu Katibu Tawala ,Mkoa wa Pwani ,Shangwe Twamala amesisitiza ulazima wa Taasisi za Umma kutumia mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa Umma “NeST” ambao unasimamiwa na mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa Umma(PPRA).Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya siku tano juu ya Mfumo wa NeST  kanda ya Pwani yaliyofanyaki Wilayani Bagamoyo.

Twamala alieleza kwamba matumizi ya mfumo huu ni maagizo ya Serikali  hivyo mahitaji  yote katika ofisi za Umma lazima yanunulliwe kwa kutumia  mfumo huo.

Alisema, waraka namba 2. wa Hazina unaotaka taasisi zote za Umma  kufanya manunuzi kupitia mfumo wa NeST.

"Pamoja na kuwa matumizi ya mfumo ni agizo la Serikali pia ni matakwa ya sheria yanayobainishwa katika sheria mpya ya ununuzi sheria no 10 ya mwaka 2023"

Twamala alielezea, mfumo huo ni rahisi na rafiki kuutumia . Pia umesaidia  kuondoa tabia za urasimu iliyokuwa ikijitokeza kipindi cha mfumo wa Zamani pia umeongeza ushirikishawaji wa watumiaji kwa kuwa wanaomba mahitaji kwa kutumia mfumo.

"Mfumo huu  wa NeST umeleta uwazi zaidi  ukilinganishwa na ule wa awali wa TANePS ambao ulikuwa na changamoto mbalimbali  ambapo ushirikishwaji ulikuwa mdogo sana na uliruhusu baadhi ya taratibu za ununuzi kufanyika nje ya Mfumo.

Katika hatua nyingine Twamala aliishauri PPRA kuweka mikakati ya kuhakikisha wanapata washiriki wengi katika mafunzo ili mfumo huu ufahamike na watumiaji wengi .

Aliipongeza PPRA kwa kuendelea kuwa wabunifu kwa kutumia wataalamu mbalimbli wa TEHAMA na sheria kuhakikisha ununuzi wa mahitaji ya Umma unafanyika kwa uwazi ili kuongeza tija katika kupata mahitaji kwa haraka na yenye thamani halisi ya fedha.

Mafunzo hayo yamewashirikisha watumiaji wa mfumo kutoka T0aasisi mbalimbali za Umma kutoka mkoani  Tanga, Morogoro na Pwani. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...