Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuriya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zasaini Mkataba wa pamoja wa Ushirikiano katika uendelezaji na Uendeshaji wa bandari kavu ambazo zitajengwa katika maeneo maalum ya Kwala - Pwani na Katosho-Kigoma kwa Tanzania na Kasambondo - Jimbo la Kalemie Tanganyika DRC; Kasumbalesa na - Jimbo la Haut Katanga DRC.

Mkataba huo umetiwa saini jijini Lumbumbashi Nchini DRC 7 Juni 2024 ambapo kwa niaba ya Serikali ya JMT umewakilishwa na Naibu Waziri Wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile na upande wa Serikali ya JKC uliwakilishwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Marc Ekila Likombo.

Akizungumza mara baada ya Hafla ya utiaji saini mkataba huo Naibu Waziri Wa Uchukuzi Tanzania Mhe. Kihenzile amesema kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatenga hekta 15 za ardhi katika eneo la Katosho- Kigoma na Hekta 45 katika eneo la Kwala- Pwani sambamba na kutoa Hati Miliki kwa ajili ya DRC kujenga na kuendesha Bandari Kavu.

Naibu Waziri Kihenzile amesema Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha usafirishaji na uchukuzi unarahisishwa hususani kwa mzigo mkubwa unaosafirishwa na DRC kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Naye Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa DRC Mhe. Likombo amesema kwa Upande wa Jamhuri yaCongo DRC Serikali itatenga Hekta 15 katika eneo la Kasumbalesa na Hekta 20 katika eneo la Kasenga-Jimbo la Haut Katanga na Hekta 25 katika eneo la Kasambondo- Kalemie Jimbo la Tanganyika sambambana kutoa Hati Miliki kwa ajili ya Serikali ya Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujenga na kuendesha bandari Kavu.

Waziri Mhe. Likombo ameongeza kuwa Serikali ya DRC imefanya hivyo ili kuimarisha mahusiano na kukuza biashara ya usafirishaji baina ya nchi hizo mbili.

Mkataba huo unatajiwa kuongeza ufanisi na idadi ya mzigo unaosafirishwa katika myororo mzima wa Uchukuzi ambapo kwa sasa takwimu zinazonyesha kwa 2022/23 tan milioni 3.5 za mzigo wa Kongo zilihudumiwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...