NYOTA wa muziki anayechipukia kwa kasi kutoka nchini Nigeria, Vasa anayofuraha kubwa kwa mashabiki zake wa muziki mzuri, kwani leo Juni 28,2024 staa huyo anatarajia kuachia EP yake mpya na ya iitwayo, "The Book of Vasa,".

EP hiyo ambayo inatoka Ijumaa ya leo ina ngoma zipatazo tano ambazo ni :- 1. Prologue, 2. Trabaye (featuring Crayon), 3. Tonight, 4. Iwomikan na 5. Osanle zimetajwa kuwa ni ngoma kali katika muziki zinazokuja kuleta mapinduzi kwa mwaka 2024 hasa kwa msanii anayechipukia.

"The Book of Vasa," ni EP iliyosubiriwa kwa hamu kubwa sana na imetoka katika wakati sahihi, "The Book of Vasa," inamkusanyo wa nyimbo zinazosisimua ambazo zimechanganya muziki wa Afrosoul na wa kisasa.

Katika kila wimbo ambao upo kwenye EP unasimulia hadithi tofauti na mashairi yake yamepangiliwa katika hali ya ustadi wa hali ya juu jambo linaloonyesha kuwa Vasa, hajaja kupoteza muda kwenye muziki kupitia EP hiyo.

Kwa ushirikiano wa timu nzima ya uzalishaji, chini ya wazalishaji mashuhuri T.U.C, Larry Lanes, Damie, na Solyshine, wanaahidi kuwa EP hii ni miongoni mwa kazi zenye ubora wa hali ya juu Kupitia

Machache kuhusu Vasa!!
Akiwa amesainiwa na Ize Records, Vasa mwenye umri wa miaka 19, aliyezaliwa Freedom Ali, amejipatia umaarufu kwa kasi katika anga ya muziki ya Nigeria. Vasa amekuwa akivutia wasanii mbalimbali kwa nyimbo zake kama vile "Bolanle," "Treasure," na "50-50," ambayo ilikusanya streams zaidi ya 200,000 kwenye Spotify na kusababisha wimbo mpya utokee kati yake na Bella Shmurda.

Safari yake ya muziki imepata msukumo kutoka kwa magwiji wa muziki kama vile Tuface Idibia, Jon Bellion, NF, Koffee, na Burna Boy, sauti ya Vasa inavuka mipaka na kuvuma kwa hadhira duniani kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...