Na Elizaberth Msagula,Lindi

Viongozi ngazi ya Wilaya na Mkoa wa Lindi wamekumbushwa kuzingatia weledi katika utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa Mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Zainab Telack amekumbusha hayo leo Juni 10, 2024 katika utambulisho wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha uuguzi Lindi.

“Niwakumbushe mambo mawili ya msingi, moja tunapaswa kuwa na weledi katika utekelezaji wa mpango huu, kwani yapo mambo mengi ambayo yanaweza kuibuka wakati wa utekelezaji hasa katika zoezi la kuchagua watoa huduma ambao kimsingi wanachaguliwa na wanajamii wenyewe “ Mhe. Ndemanga.

Ndemanga ametumia pia fursa hiyo kuwakumbusha wataalam juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu vizuri, ambazo zinasaidia sana kuondoa sintofahamu wakati wa utekelezaji na baada ya utekelezaji wa kuwapata watoa huduma ngazi ya jamii na shughuli zingine muhimu za kiutendaji.

“ Bila shaka mnafahamu juu ya umuhimu wa kumbukumbu, hivyo katika zoezi hili tunapaswa kuzingatia kuweka kumbukumbu sawa kama ambavyo mazoezi mengine yalivyofanyika vizuri “Alisema Ndemanga.

Kwa upande wake Bi. Orsolina Tolage ambaye ni Afisa progamu wa mpango wa Huduma za Afya ngazi ya jamii kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma ameeleza malengo ya mpango huo kuwa ni pamoja na kuzuia magonjwa yasiyo ambukiza kama vile Malaria, Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora pamoja na magonjwa yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Na Afisa Maendeleo ya Jamii idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais –TAMISEMI Ndugu Jeremiah Mwambange akieleza muongozo wa utaratibu wa kuwapata wahudumu wa Afya ngazi ya jamii amesema kuwa, jamii ndiyo yenye jukumu la kumchagua mhudumu wa Afya ngazi ya jamii kadri watakavyoona anafaa kuwahudumia kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa .

Serikali imeweka utaratibu wa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahudumu tajwa kupitia vyuo vya Afya vya kati na hatimaye kuwawezesha kutekeleza majukumu ngazi ya jamii kwa kuwapa vitendea kazi na motisha.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...