Raisa Said,Tanga
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewataka viongozi na watendaji wa chama hicho kuongeza umakini katika zoezi la usajili wa wanachama kieltroniki na utoaji wa kadi kwa lengo la kuzuia usajili holela wa watu ambao wanasajiliwa kwa ajili ya kura za maoni tu. .
Tahadhari hiyo imetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Selemani Sankwa alipokuwa akifunga mafunzo ya siku moja ya Sensa ya Watu na Makazi kwa ajili ya wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT), Mkoa wa Tanga. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Usagara, jijini Tanga.
Sankwa alisema kuwa hivi sasa kuna watu wanawania kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika chaguzi mbalimbali, hivyo wasipokuwa makini kuna watu watapata kadi kiholela na huku Katibu wa Tawi au wa Wilaya akiwa hajui,
“Watu hao ni wale ambao baada ya kura za maoni wanarudisha kadi kwa wapinzani wakidai wamejitoa CCM,” alisema na kuahidi kuwa wanafuatilia zoezi hilo kwa karibu na kuhakiki kadi hizo ili kusiwe na utoaji wa kadi kiholela.
Akizungumzia kwa ujumla juu ya zoezi la usajili wa wananchama kieletroniki alisema kuwa bado zoezi hilo halijakuwa la kuridhisha.
“Tunalenga kusajili wanachama 100,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu na tumesajili wanachama 27,000 hadi mwezi Machi,” alieleza.
Aliwataka viongozi wote kupanga mikakati ya kuongeza simu za usajili ili kuongeza kasi ya usajili. Akaeleza kuwa wanafuatilia kwa ukaribu zoezi hilona kila siku matokeo ya usajili yanawekwa katika Group la Whatsap ya Halmashauri Kuu ya Mkoa.
Alisema kuwa wilaya za Handeni, Muheza na Lushoto zimekuwa zikifanya vizuri, lakini kwa mwezi Mei, Tanga wamefanya vizuri kwa kusajili wanachama 1,000.
Pia aitoa wito mahususi kwa viongozi na watendaji wa UWT kupanga mikakati ya kuongeza simu kwa ajili ya kuongeza kasi ya usajili wa wanachama.
Sankwa pia aliwataka viongozi wote waliopata mafunzo kuhakikisha waliyojifunza yanafika ngazi ya chini. Alisema kuwa kuanzia wiki inayokuja Kamati ya Utengaji ya mkoa itaanza ziara kwa jili kuhakiki zoezi hilo.
Aliwahimiza kuwahamasisha watu wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kuboresha na kujiandika kaika daftaril a wapiga kura wsikose haki ya kuchagua viongozi katika ngazi mbalimbali .Katibu wa UWT wa Mkoa wa Tanga, Aziza Hussein Kiduda alisema kuwa wamepanga kusajili wanachama 300,000 hadi kufikia mwisho wa mwaka huu.
Alisema hadi hivi sasa wamekwishasajil wanachama 3,528 na wanategemea kuongeza kasi ya usajili ili wafikie lengo walilojiwekea.
Hate hivyo katibu huyo aliwapomgeza wa bunge wa viti maalum mkoa wa Tanga kwa kugawa simu kwaajili ya usajili wa wanachama.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...