Waathirika wa Maafa ya Kimbunga " Hidaya" wilayani Mafia wameanza rasmi kupokea misaada kwa kata mbili ya Kiegeani na Miburani.

Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia, Olivanus Thomas amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kutenga fedha milioni 71 kwa ajili ya waathirika wa maafa wilayani Mafia.

" Rais aliielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kuipatia wilaya ya Mafia Shilingi Milioni 71 kwa ajili ya ununuzi wa chakula ambapo ni unga na maharage, hivyo kuguswa kwa Rais wetu kunahitaji pongezi.

Aidha, Thomas amewapongeza wadau mbalimbali kutoka nje na ndani ya Mafia waliojitokeza kusaidia waathirika wa maafa. 

Misaada iliyoanza kukabidhiwa kwa kata za Kiegeani na Miburani kwa ujumla ni pamoja na magodoro 167, blanketi 247, na vifaa vya usafi.

Walengwa wa misaada hiyo ,akiwemo Latifa faustin wameishukuru na kupongeza Serikali pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kwa ajili ya wilaya ya Mafia.

" Namshukuru Mungu na Serikali yetu kwa msaada mkubwa, Mungu awabariki na uongozi usirudi nyuma, uzidi kusonga mbele na kujali sana wananchi" alisema Latifa Faustin.

Zoezi la ugawaji wa misaada linatarajiwa kuendelea kwa kutembelea wahanga waliopo katika kata za Baleni, Kirongwe na Kilindoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...