Na Mwandishi Wetu

Serikali kupitia Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) imeendelea kutoa mbinu  za kupunguza migogoro katika sekta ya ujenzi na  nyinginezo, kupitia mafunzo yanayoandaliwa na Baraza hilo.

Kwa siku tatu mfululizo kuanzia Juni 26, mwaka huu, Baraza la Taifa la Ujenzi limeendesha mfunzo ya utatuzi wa migogoro nje nje ya mahakama kwa wadau mbalimbali wa Sekta hiyo, wafanyabiashara na hata wanasheria.

Hatua hiyo inaelezwa kusaidia upatikanaji wa suluhu ya migogoro kwa namna rafiki inayotoa fursa kwa pande mbili husika  kuelewana bila kwenda Mahakamani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akitoa mafunzo hayo   yamayoratibiwa na Baraza la Taifa la Ujenzi,  Mkadiriaji Majenzi wa NCC, Bw. Elias Kissamo, amesema wana amini kuwa yatawasaidia washiriki kuwa na uelewa mpana wa njia bora za kutatua migogoro katika shughuli zao, badala ya kupelekana mahakamani.

Bw. Kissamo amesema Baraza la Taifa la Ujenzi limeundwa kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya Sekta ya Ujenzi nchini, ikiwemo kuwa na njia sahihi za kusimamia usuluhishi wa migogoro nje ya mahakama.

“NCC  inaratibu na kusimamia usuluhisi wa migogoro katika Sekta ya Ujenzi na si msuluhishi.

... Kazi ya Baraza ni pamoja na  kuchagua wasuluhishi miongoni mwa waliopo kwenye mpangilio ili washughulike na utatuzi wa mgogoro unaotakiwa kutatuliwa', amesema Bw. Kissamo.

Naye Rais wa Chama Cha Mawakili Afrika Mashariki, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt. Fauz Twaib, amesema kutokana na kuwepo kwa migogoro imeonekana kuwe na mfumo mbadala wa mahakama kutatua migogoro.

Amesema kuna mambo mengi yanayoweza kuepukwa kwa kutumia mfumo nje ya mahakama.

 Amesema hiyo itasaidia kupunguza matumizi ya muda mahakmani, gharama mbalimbali, pamoja na kuwaacha wahusika wote katika uhusiano mwema.
Kwa upande wake, Mshiriki wa mafunzo hayo, Wakili wa Serikali, Bi. Rehema Mtulya, amesema mafunzo hayo yatamsaidia kuendesha mashauri ya usuluhishi kwa weledi zaidi.

Bi. Mtulya ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuhudhuria mafunzo hayo kwani yanakwenda kupunguza migogoro katika sekta ya ujenzi na nyingine nchini.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...