Naibu Katibu Mkuu anayesimamia miundombinu OR-TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila amewataka Wahandisi Washauri wanaosimamia miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara nchini kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.

Mhandisi Mativila ameyasema hayo leo tarehe 10 Juni,2024 wakati akikagua ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi katika manispaa ya Tabora ambalo lipo chini ya mradi wa TACTIC unaosimamiwa na TARURA.

“Mhe. Rais Dkt. samia Suluhu Hassan anahangaika kutafuta fedha ili kuhakikisha wananchi wanapata barabara,wataalam lazima mbadilike  na kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa miradi hii.

Mkandarasi huyu angekuwa anasimamiwa kwa ukaribu angeshakuwa amemaliza hapa”.

Hata hivyo Mhandisi Mativila amewataka wataalam hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa ujenzi ili wakandarasi wakamilishe kazi kwa wakati.

Aidha, amemtaka Mhandisi Mshauri UNITEC  Civil Consultants ltd kuhakikisha anasimamia kwa karibu ujenzi huo na ifikapo mwezi Agosti mwaka huu jengo hilo liwe limekamilika.

Ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi linalogharimu takriban milioni 800 lilianza ujenzi wake Novemba 2023 na lilitarajiwa kukamilika 15 Juni,2024 na kuagiza ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Agosti 2024 na linajengwa na mkandarasi CICO Contractor.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...