Na Mwandishi wetu,Nyasa

BAADHI ya wananchi wa vijiji vinavyopitiwa na barabara ya Unyoni –Liparamba  hadi Mkenda mpakani mwa Tanzania na Msumbuji wilaya ya Nyasa ,wameishukuru Serikali kupitia wakala wa barabara Tanzania(TANROADS)kwa kuanza ujenzi  wa barabara hiyo ambayo miundombinu yake imeharibiwa vibaya na mvua za masika.

Leonald Kawonga mkazi wa Liparamba amesema,wakati wa masika barabara hiyo  ilikuwa changamoto kubwa kutokana na utelezi na magari kukwama,hivyo matengenezo hayo yatawezesha  kupitika kirahisi na kutumika kwa ajili ya usafiri na usafirishaji wa mazao kutoka mashambani kwenda sokoni.

Lenatha Haule,ameishukuru TANROADS kwa uamuzi wa kufanya matengenezo barabara hiyo,kwani katika kipindi chote cha masika baadhi ya shughuli nyingi  za kujiingizia kipato zilisimama kutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya uhakika.

Alisema,barabara hiyo ilikuwa haipitiki kirahisi baada ya kuharibika vibaya na mvua zilizonyesha kwa wingi hasa katika wilaya ya Nyasa,hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya barabara kukatika na wananchi hao kutokuwa na uhakika wa mawasiliano pindi wanapotaka kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Mkazi wa kijiji cha Kingerikiti Zawadi Nyondo amesema, barabara hiyo ina umuhimu mkubwa kwa sababu ndiyo inayotengeneza mapato makubwa katika wilaya ya Nyasa kutokana na ukanda huo kuwa yenye uzalishaji mkubwa wa mazao hasa  Kahawa,mahindi na maharage.

“barabara hii ni tegemeo kubwa kiuchumi kwetu sisi wananchi wa wilaya ya Nyasa na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla,lakini miundombinu yake bado ni dhaifu,tunaiomba serikali ione namna ya kuijenga kwa kiwango cha lami badala ya kuendelea kufanya matengenezo mwaka hadi mwaka kwa kiwango cha changarawe”alisema.

Kwa mujibu wa Nyondo,barabara hiyo ilipochukuliwa na TANROADS zaidi ya miaka kumi iliyopita walikuwa na matumaini makubwa kwamba itejengwa kwa kiwango cha lami ili kuwaondolea adha hasa wakati wa masika,lakini hadi sasa  bado ya changarawe na wanaendelea kuteseka kutokana na ubovu wake.

Mkazi wa kijiji cha Lumeme Timoth Mapunda,ameiomba serikali kupitia TANROADS kutengeneza upya baadhi ya madaraja yaliyopo kwenye barabara hiyo ili kuruhusu maji kupita chini ya madaraja,badala ya juu ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa watu kusombwa na maji.


Muonekano wa  barabara ya Unyoni-Liparamba-Mkenda inayofanyiwa matengenezo baada ya kuharibika na mvua za masika.
 Kazi ya matengenezo ya barabara hiyo ikiendelea.

Wahandisi kutoka wakala wa barabara Tanzania (TANROADS)) Mkoa  wa Ruvuma Peter Ndalemya kushoto  na Juma  Mkela wakikagua ujenzi wa Reli katika barabara ya Unyoni-Liparamba-Mkenda ambayo baadhi ya maeneo  ya barabara hiyo imeharibika kutokana na mvua za masika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...