WASANII 08 vya Wanufaika na Mradi wa mfuko wa fedha wa kuwawezesha Wasanii (FEEL FREE GRANTEES) kwa mwaka 2024 Wasaini rasmi Mikataba ya kupata fedha za miradi yao.

Akizungumza na Wanahabari Ofisi za Taasisi ya Nafasi arts space Mikocheni Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa (BASATA) Edward Buganga ametoa pongezi kwa Taasisi ya Nafasi arts space kwa kufanya utafiti na kuvumbua vipaji vya wasanii wa Sanaa zote bila kubagua na kuwapa kipaumbele cha kupata fedha kwa ajili ya kuboresha miradi kazi yao ya kisanii.

Hata hivyo Buganga ametoa wito kwa wasanii hao kuhakikisha wanafanya kazi hizo kisheria na kutambulika na Baraza hilo (BASATA) Kwa Kuhakikisha wanafika na kujisajiri ili .

Pia amewataka wanufaika hao kutumia fedha hizo kwa lengo lilimokusudiwa ili kujenga imani kwa wafadhili hao kuendelea kusaidia na wasanii ambao watakuja siku za usoni kuhakikisha Sanaa inakuwa na kujitangaza.

Nae Mkurugenzi wa Bodi ya Taasisi hiyo Paul Ndunguru amesema walipokea mombi ya kuwezeshwa wasanii hao kifedha zaidi ya 100 lakini walifanya mchujo na kupata watu 08 ambao walikidhi vigezo vya kupata kuwezeshwa kutokana na mpango kazi wao ambao waliweza kuwasilisha kwa njia ya Maandishi (PROPASAL).

Ndunguru ameongeza kuwa Mfuko huo haukopeshi Msanii bali unampatia fedha ambayo itamuwezesha kufanya mradi huo na baadae kumtafutia masoko ya kazi yake pale itakapotamatika .

"Kama tunavofaham mradi huu umekuwa ukidhaminiwa na nchi ya Norway pamoja na nchi ya Swizz kwa pamoja kwa kushirikiana na Taasisi ya Nafasi arts space,mfuko huu hauna lengo la kukopesha msanii au kuweka dhamana yake yoyote kama Masharti ya baadhi ya mifuko ambapo imekuwa inaleta mkanganyiko na kupelekea Msanii asioneshe Kazi yake inavotakiwa kutokana na masharti hayo hivyo sisi Kama Nafasi tunapokea maombi ya wasanii hao wakiwa na miradi yao tunawapa nafasi ya kuonesha hadhira kisha tunamtafutia masoko ya kuuza kazi yake hiyo."

Mmoja ya Wafaidika wa Mradi huo Mtayarishaji Mkongwe wa Kazi za Filamu nchini Tanzania Amir shivji amesema kupitia mradi kazi wake "Kaburi wazi" ameweza kuwa mnufaika wa fedha hizo na kuhaidi kutengeneza kazi nzuri na zenye ubora kutokana na mradi kazi wake kulenga zaidi tamaduni za kijerumani.

Vikundi vingine vilivyofaidika na fedha hizo ni pamoja na Asedeva,Ally Baharoon,Mihayo Kallaye,Dinembo, Lilian Munuo ,Ekande ,Thobias Minzi pamoja na Kikundi cha Bwagamoyo Africulture.

 

Wanufaika 08  kupitia Mradi wa "Feel Free grantees " wakisikiliza maneno mawili matatu kutoka kwa uongozi wa Taasisi ya Nafasi Arts space mara baada ya kukabidhiwa kwa mikataba yao mapema Leo Juni 06,2024 Mikocheni Jijini Dar es Salaam
 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nafasi arts space Lilian Hipolyte akimkabidhi Mkataba mmoja ya Wanufaika 08 wa Mradi wa "Feel Free"  Dinembo mwenye Mradi kazi wa sanaa za tattoo  mapema Leo Juni 06,2024 katika Ofisi za Taasisi hiyo  Mikocheni Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...