WAKATI Maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Kibishashara yakiendelea kushika kasi katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Kituo cha Mikutano APC Hotel and Conference Centre kimepongezwa kwa kuendelea kutoa Elimu jinsi ambavyo kituo hicho kimeendelea kutoa huduma kwa Jamii pamoja na kuzalisha ajira mbalimbali kwa vijana Nchini.
Hayo yamebainishwa leo Julai 06,2024 na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S.Temu wakati alipo tembelea banda la Kituo hicho katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere
Amesema Kituo hicho cha APC kimekuwa kikitoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za hoteli, kumbi za mikutano zenye uwezo wa kubeba watu wengi.
Aidha CPA Prof. Sylvia Temu amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikitoa Fursa za ajira kwa vijana na kuwataka watanzania kuendelea kuchangiamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kuweza kujikwamua kiuchumi
Katika hatua nyingine CPA Prof. Sylvia Temu ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kutembelea banda hilo ilikujionea jinsi ambavyo Kituo hicho kimekuwa kikiendelea kuvutia wawekezaji kupitia huduma mbalimbali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Shirika kutoka NBAA CPA Kulwa Malendeja wakimsikiliza Afisa Masoko kutoka APC Hotel Conference Center Happy Sanga kuhusu kazi zinazofanywa na Kituo hicho katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Mikutano APC Hotel and Conference Centre katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Kituo cha Mikutano APC Hotel and Conference Centre katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea Banda la Kituo cha Mikutano APC Hotel and Conference Centre katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa APC alipotembelea Banda la Kituo cha Mikutano APC Hotel and Conference Centre katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...