Na Leandra Gabriel, Dar es Salaam
RAIS wa Marekani Joe Biden amejiengua katika kinyang’anyiro cha kuwania muhula wa pili wa kiti cha urais na kueleza kuwa atahudumu katika kipindi chake cha urais kilichobaki.
Kupitia ukurasa wake wa X awali Twitter Biden ametangaza uamuzi huo na kueleza kuwa amefikia uamuzi huo kwa manufaa ya chama cha Democrats, na ni fahari ya maisha yake kuhudumu kama Rais, na kumshukuru Makamu wa Rais Kamala Harris kwa ushirikiano mkubwa aliompa.
Aidha Biden ameeleza kuwa, atazungumza na Taifa hilo baadaye wiki ijayo kwa undani zaidi.
Biden amejiengua katika mbio urais ikiwa imesalia miezi minne pekee kabla ya Taifa hilo kuingia katika uchaguzi mkuu.
Biden amekuwa akishinikizwa na wanachama wa chama anachokiwakilisha kujiondoa katika mbio hizo za urais baada ya kutofanya vyema katika mdahalo uliowakutanisha na mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Republican Donal Trump.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...