Na Mwandishi Wetu

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameitaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuiwezesha Mahakama nchini kuunganishwa kwenye Kanzidata ya Wakala ili kuweza kuhakiki taarifa za kampuni kwa uharaka pindi inapokuwa inashughulikia mashauri yahusuyo kampuni hizo

Rai hiyo ameitoa leo tarehe 5 Juni, 2024 alipotembelea banda la BRELA lilipo ndani ya jengo la Wizara ya Viwanda na Biashara katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam.

Prof. Ibrahim Juma amesema kuwa uunganishwaji katika kanzi data itaiwezesha Mahakama kujua uhai wa kampuni na endapo imehuisha taaifa zake kwa Msajili hii itasaidia kuamua kuendelea na kesi au kusitisha endapo kampuni haijahuisha taarifa zake kwa Msajili

Aidha, Jaji Mkuu ameipongeza BRELA kwa kazi kubwa inayofanya katika kuboresha utoaji wa huduma zake kwa njia ya mtandao

BRELA inashiriki katika kutoa huduma za papo kwa hapo kwenye maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam ndani ya banda la Wizara ya Viwanda na Biashara na banda karibu na Wizara ya Fedha na Mipango .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...