BODI ya Kahawa Tanzania, imeendelea kuhamasisha jamii kuhusu unywaji kahawa.

Hamasa hiyo imetolewa leo katika uzinduzi wa Kampeni ya wapanda mlima na waendesha baiskeli wa Mlima Kilimanjaro.

Uzinduzi wa kampeni hiyo iliyolenga kupambana na kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini, umefanyika katika geti la Machame.

Akizungumza katika hafla hiyo, afisa usimamizi ubora wa Bodi ya Kahawa, Anastasia Shirima, amesema bodi imejiwekea lengo la kuongeza unywaji wa kahawa ili kufikia asilimia 15 ya kahawa yote inayozalishwa nchini.

Wapanda Mlima hao wanatarajiwa kushuka kileleni ifikapo Julai 25, mwaka huu, ambapo watapokelewa katika geti la Mweka.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...