Na Mwamvua Mwinyi,Mafia - PWANI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mhe. Subira Mgalu amekabidhi vyerehani kumi na moja (11), vyenye thamani ya Tsh. 3,300,000/- kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wilayani Mafia, kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi.
Vyerehani hivyo amevitoa ikiwa ni ahadi yake aliyoiahidi wilayani humo, na amelenga kuwanyanyua kiuchumi wanawake wa Jumuiya hiyo katika Kata zake zote nane.
"Fani ya ushonaji inaongoza kwa kipato, wakijipanga watafanikiwa," Mhe. Mgalu amesema.
Aidha, ametoa rai kwa Jumuiya hiyo wasigombane, na washirikiane kwa kuwa amewapa vyerehani hivyo kwa umoja wao kwa ajili ya kujiwezesha wenyewe, ili kuwezesha shughuli za UWT katika wilaya hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...