Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya ametembelea banda ya Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Bw. Mwandumbya alifahamishwa na watumishi wa PPAA kuhusu majukumu ya PPAA ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa moduli mpya ya uwasilishaji wa malalamiko/rufaa kwa njia ya kieletroniki.

Naibu Katibu Mkuu alitembelea banda la PPAA hivi karibuni alipofanya ziara ya kujionea Maonesho ya Sabasaba yaliyoanza 28 Juni - 13 Julai, 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...