Dkt. Kikwete ametoa pongezi hizo leo alipotembelea banda la FCC lilipo ndani ya Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo huduma za elimu na majukumu ya FCC zinatolewa kwa wadau na wananchi wanaotembelea banda hilo.
"Watanzania wakipata elimu hii ya bidhaa bandia itasaidia sana kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na kusaidia kukua kwa biashara na ushindani katika soko na wananchi watapata bidhaa halisi na salama” amesema Dkt. Kikwete.
Aidha, Dkt. Kikwete amewapongeza wafanyakazi wa FCC kwa kazi nzuri wanazofanya hususan utoaji wa elimu ambapo hizo zitawasaidia wananchi hao kupata uelewa wa kina katika kutambua bidhaa bandia.
Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Kurasini Jijini Dar es Salaam yalifunguliwa rasmi na Mhe. Mhandisi. Filipe Jacinto Nyusi, Rais wa Msumbiji akiwa na mwenyeji wake Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani tarehe 3 Julai, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...