Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Halmashauri ya wilaya ya Songea kuhakikisha daraja la Lumecha linajengwa ndani ya kipindi kifupi na kwa ubora.

Waziri ametoa kauli hiyo leo tarehe 10/07/2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea Miradi ya maendeleo katika kijiji cha Liweta Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

“Serikali imetoa kiasi cha Millioni Mia nne kujenga Madaraja na akiba ya fedha itakayobaki itatumika kutengeneza barabara mpaka kijiji cha Liweta ikiwa ni pamoja na kufukia shimo lilopo katika barabara hiyo alisema,” Waziri Mhagama.

kazi ya ujenzi wa barabara ni kazi muhimu naomba wananchi msaidie katika kulinda mradi ili ujenzi ili ukamilike kwa wakati na tufungue njia zitakazochochea uchumia katika kijiji cha Liweta.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza na wananchi wa Liweta katika Mkutano wa hadhara kuhusu ujenzi wa Daraja la Lumecha unatarajia kuanza hivi karibuni.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...