SHINDANO la Wazi la Mchezo wa Gofu "Vodacom Lugalo Open 2024"limeanza rasmi leo kwa Wachezaji wa Ridhaa na wa Kulipwa katika Klabu ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Mapema Leo Julai 05,2024 Viwanja vya Klabu ya Lugalo gofu Jijini Dar es Salaam Meja Japhet Masai Nahodha Wa Klabu Ya Lugalo amesema, Muitikio umekuwa Mkubwa katika siku ya kwanza ukilinganisha na Ukubwa wa Shindano Hilo na wanategemea ushindani kuongezeka katika siku nyengine mbili za mashindano.

"Leo imekuwa siku ya kwanza ya Shindano hili hivyo tunategemea siku ya Kesho na Keshokutwa yatafungwa mashindano haya lakini Shindano hili limeshirikisha daraja la A, Wachezaji mahiri na Wachezaji wa Kulipwa''.

Hata hivyo Nahodha huyo ameongeza kuwa Viwanja vipo vizuri na Vinachezeka Kwa uzuri na Wachezaji wote waliojiandikisha wameweza kufika wote kwa muda hivyo Shindano kwa siku ya kwanza limefanikiwa na limeweza kuisha kwa wakati.

Pia ameendelea Kuwashukuru Wadhamini hao wa Shindano hilo Vodacom pamoja na wadhamini wengine walioweza kuunga Mkono Shindano hilo huku akiwataka Wachezaji waweze kufata sheria na huku anatagemea Ushindani utakuwa mkubwa kutokana na vilabu vyote nchi nzima kuleta Wachezaji.

Kwa Upande Wake Jumanne Mbunda Mchezaji wa Lugalo Gofu ameongoza Kwa siku ya kwanza Kwa Mikwaju 74 amesema,Siri ni mazoezi na Nia ya Dhati ya Mchezo ndio imefanikisha aweze kushika Usukani Kwa siku ya kwanza.

"Viwanja vimewekwa tayari kwa ajili ya Shindano hili hivyo hatukuweza kukutana na changamoto ya upepo wa Asubuhi na ndio sababu imefanya niweze kucheza vizuri kwa siku ya kwanza pamoja na Waandaaji wa Shindano hilo Vodacom Kuandaa vizuri."

Nae Nahodha kwa Upande wa Wanawake Hawa Wanyeche Kila Mchezaji amekuwa na Ari ya Kucheza vizuri na Viwanja Vimeandaliwa vizuri Kwa ajili ya Mashindano haya.

"Kila mtu anatamani kukaa kwenye Nafasi nzuri hivyo tunategemea Matokeo siku ya Mwisho ambayo itakuwa kilele chake hivyo tutajua ambae ameibuka Mshindi ."

Pia amewaalika wapenzi wa Michezo Kufika Viwanja hivyo Kushuhudia Mashindano hayo ya siku 03 ambayo yameanza rasmi Leo.

Aidha Klabu Mbalimbali Zimeshiriki Shindano Hilo Ikiwemo, Arusha Gymkhana,Dar Gymkhna,Morogoro Gymkhana,Moshi,TPC moshi,Mufindi Golf Nawenyeji Lugalo Golf Klabu ambapo Mashindano hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 07,2024 Viwanja vya Klabu ya Lugalo gofu Jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...