MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) imewataka Watanzania kuchangamkia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika viwanja vya ndege nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Fedha wa TAA, Shadrack Chilongani, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAA ambapo amesema kuwa wameshiriki Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), maalum kwa ajili ya kuwaeleza wananchi shughuli zinazofanywa na TAA sambamba na fursa zilizopo.

"Katika eneo la Usafiri wa Anga kuna Mamlaka mbalimbali zinazoendesha shughuli zake na zinategemeana ambao ni Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) pamoja Shirika la Ndege nchini (ATCL) ili kuhakikisha huduma za usafiri wa ndege hivyo ni vyema wadau wengine kujitokeza ili kuweza kukuza na kuendeleza Usafiri wa Anga hapa nchini kwa kuwa ni fursa." alisema CPA Chilongani

Amesema TAA inasimamia na kuboresha viwanja 59 vya ndege na kati ya hivyo viwanja 14 vina miundombinu thabiti ya uwekezaji kama lami na miundombinu mingine wezeshi hivyo wingi wa viwanja hivyo wanahitaji wadau kuja kuwekeza kwenye viwanja hivyo.Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TAA Bw, Juma Hassan Fimbo pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shadrack Chilongani aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAA wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mipango na Takwimu kutoka TAA Edward Kimaro walipotembelea Banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) lilopo katika jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shadrack Chilongani akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TAA Bw, Juma Hassan Fimbo alipotembelea alipotembelea Banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) lilopo katika jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shadrack Chilongani akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) katika jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shadrack Chilongani akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) alipotembelea Banda la chuo hicho lililopo kwenye jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shadrack Chilongani akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko na Biashara ATCL Jerry Ngewe alipotembelea jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shadrack Chilongani akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) alipotembelea Banda la chuo hicho lililopo kwenye jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Biashara CPA Shadrack Chilongani aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAA akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) alipotembelea jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...