BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua huduma mpya ya akaunti ya kidigitali (TCB POPOTE ACCOUNT ) ambayo itakayomfanya mteja alipie bili mbalimbali kupitia simu yake ya mkononi akiwa sehemu yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika leo Julai 30, 2024 katika ofisi za TCB Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko Ukuzaji wa Biashara na Mahusiano ya Umma, Deo Kwiyukwa amesema huduma hiyo ya akaunti ya kidigitali unaweza  ukalipia bili mbalimbali na ukanunua tiketi ya treni ya Mwendokasi katika App ya TCB na gharama ya kujiunga na TCB POPOTE ACCOUNT ni shilingi Elfu moja.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha  Ufumbuzi wa Kigitali wa TCB Jesse Jackson amesema wanatarajia kuwafikia wateja wapya 250,000  ifikapo Desemba mwaka huu kupitia huduma yao ya ‘TCB Popote’ ambayo itawawezesha wananchi kufungua akaunti kidigitali.

“Malengo yetu kwakipindi cha  miezi minne iliyobaki tunataka  kuwafikia wateja laki mbili na nusu  ambao watafungua akaunti hizi zakidigitali kupitia simu janja zao,malengo ya mbele zaidi ambayo yataanzia mwakani ambapo tutakuwa tumeshaweka maandalizi kwa ajili ya simu za kawaida tunatarajia kufikia wateja wengi zaidi,”amesema Jackson.

Pamoja na hayo amesema huduma hiyo ni mwendelezo wa ubunifu unaofanywa na benki hiyo kwakuwa kwa miaka kadhaa TCB imekuwa  ikifanya bunifu ili kuleta huduma karibu na wateja.

Amesema lengo lao ni  kuwaleta wateja karibu  kwakuwa wao ni benki ya tatu kwa matawi na mpaka sasa wana mawakala  6000 Tanzania nzima.

“Tumeona hiyo  haitoshi tunahitaji kusogeza huduma  za kifedha kwa  wananchi kwakuwa takwimu zinaonesha asilinia 89 ya watanzania wanaweza kupata huduma  za kifedha ndani ya kilomita tano na  asilimia 22  tu ya Watanzania wana akaunti zakibenki,”amesema Jackson.

“Huduma  hii ya TCB Popote inafanya  mtu anaweza kufungua akunti popote alipo anachohitaji ni simu janja yake na kitambulisho,akaunti hii ikikamilika itaweza kutoa huduma ya kulipia bidhaa mbalimbali na huduma za mikopo,”amesema.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...