Na Chalila Kibuda , Michuzi TV

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA), imeandaa mbio ‘marathon’ kwa ajili ya kutunisha mfuko kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wenye uhitaji.

Mbio hizo zimebuni na Chuo baada ya kuona baadhi ya wanafunzi wanashindwa kuendelea na masoma ikiwemo ada pamoja na walio na mahitaji maalumu kama vile watu wenye ulemavu.

Hayo ameyasema Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo wakati katika Banda la TIA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF)

Mbio hizo zitazinduliwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba Oktoba 26 mwaka

Amesema taasisi hiyo imebaini kwamba wapo wanafunzi ambao wanafanya vizuri katika masomo, huku baadhi yao walishindwa kumudu gharama za masomo wakiwamo wanafunzi akihamasisha wadau wengine waunge mkono maandalizi ya mbio hizo na kufanisha wanafunzi walio wenye mahitaji kupata elimu.

“Tunaandaa ‘TIA Marathon’ zitafanyika Oktoba 26, mwaka huu na tutafanya ufunguzi rasmi mwezi huu, sehemu ya pesa itakayopatikana itawasaidia wanafunzi wetu ambao tangu shule ya msingi walipata fursa ya kusoma hadi sekondari kwa ufadhili wa serikali, wanakwama huku juu.

“Tunalenga kuunga mkono serikali kwa namna anavyosaidia vijana kupata elimu, kuwasaiadia ambao hawana uwezo wa kulipa ada, kununua vifaa maalum vya kujifunzia walio na mahitaji maalum.

“Lakini Kuna kundi ambalo wanafunzi wamenza familia ila hawana uwezo wanahitaji kusoma, awe na mlezi wa mtoto na amlipe.

Prof. Pallangyo amesema taasisi hiyo pia wamwandaa kongamano la tatu la Kimataifa jijini Arusha, Novemba mwaka huu, litakalofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko na kuhudhuriwa na nchi tofauti.

Amesema kongamano hilo ni la Kitaaluma ambapo litakuwa na wadau mbalimbali.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Pallangyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana uandaji wa mbio pamoja na kongamano akiwa katika Banda la TIA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara  Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Pallangyo akimhudumia mwananchi katika Banda la TIA  kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara  Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Pallangyo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na watumishi wa TIA  katika Banda la TIA  kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara  Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Pallangyo akizungumza na watumishi wa TIA  katika Banda la TIA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara  Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...