Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Moshi
WANUIFA wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mkoani Kilimanjaro ambao kwa sasa wanajimudu kimaisha baada ya kuwezeshwa kifedha na Mfuko huo wamesema kwa sasa wako tayari kuondolewa ili wengine wasio na uwezo wasaidiwe.
Wakizungumza na Wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ya wanufaika wa mfuko huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameeleza kwamba kupitia fedha ambazo wamepatiwa na TASAF zimewasaidia katika kufanya maendeleo pamoja na kuwa na uhakika wa kula.
Wamesema wakati wanaingizwa katika Mfuko huo walikuwa katika wakati mgumu kwani hata uwezo wa kula mlo mmoja kwa siku ilikuwa ngumu lakini baada ya kuanza kupata fedha za TASAF maisha tap yalianza kubadilika na sasa wanaamini wanaweza kuendesha maisha nje ya Mfuko kwani wengi wao wamekuwa wajasiriamali pamoja na kuwa na vikundi vya kuweka fedha na kukopa.
Wamesema kufanikiwa kwao mbali ya fedha ambayo wamekuwa wakipewa na TASAF pia wamekuwa wakipatiwa elimu ya ujasiriamali na utunzaji wa fedha ambayo kwa sehemu kubwa imewafanya kuwa na uwezo wa kumudu maisha Yao.
Akizungumza na Wahariri na waandishi hao Mnufaika wa Mfuko huo Veneria Agusti (56), mkazi wa mtaa wa Relini uliopo Kata ya Boma mbuzi l katika Manispaa ya Moshi ambaye anasema yuko tayari kuondolewa kwenye mpango wa TASAF baada ya hali yake kiuchumi kuimarika.
Amesema anaishukuru TASAF kwa msaada mkubwa ambao wamempatia kwani amefaida na uwepo wa Mfuko huo huku akisimulia hali ngumu ya maisha aliyokuwa akiishi kabla ya kuingizwa katika mpango wa Mfuko.
Pia amesema elimu ya ujasiriamali na utunzaji wa fedha ambayo ameipata kutoka TASAF imemuwezesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutunza fedha, kufanya biashara ndogo ndogo, kufuga kuku hadi kujenga nyumba nzuri ya kuishi.
Akielezea zaidi Veneria Agusti anasema alianza kupokea Sh.46000 kutoka TASAF ambazo zilimwezesha kununulia chakula na kusomeshea wanae lakini baadae aliweza kuhifadhi fedha kidogo anayopokea na kuanzisha mradi wa kufuga kuku wa kienyeji.
"Kupitia ruzuku ya TASAF nimeweza kufuga kuku, nikaanzisha mradi wa kuuza maandazi na kitembeza mtaani, baadae nikajiunga kwenye kikundi ambacho tulisaidiwa na wataalam wa TASAF ambapo tunawekeza hisa, tunakopeshana na baadae tunagawana faida, hii imenisaidia sana kumudu maisha yangu tofauti na mwanzo," anasema.
Anasema hivi karibuni alipokea ruzuku ya 350,000 kutoka TASAF ambapo anatarajia kutumia fedha hiyo kuanzisha mradi mkubwa wa kufuga kuku wa kisasa ambao utaweza kumuingizia fedha nyingi zaidi.
"Nawashukuru sana TASAF kwa namna ambavyo wamekuwa wakiwezesha kaya masikini kupata msaada wa kuinuliwa kiuchumi, nimekuwa nikipokea fedha ambazo zimeniwezesha kubadilisha maisha yangu.
"Nitumie nafasi hii kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha hizi kupitia Mfuko huo.Na kwa hali niliyonayo niko tayari kuondolewa ili wengine nao wasaidiwe.
Kwa upande waka Federika Swai ambaye ni mmoja ya wanufaika wa TASAF anayeishi kaya ya Boma Mbuzi katika Manispaa ya Moshi anasema kabla ya kuingizwa katika mpango wa Mfuko huo alikuwa anaishi maisha magumu.
"Ugumu wa maisha ulinifanya nifikirie yofauti kwasababu nilishakata tamaa ya maisha, lakini baada ya kuingizwa TASAF maisha yangu yalianza kubadilika kidogo kidogo ,nikaanza kufanyabiashara ndogondogo na kufuga ng'ombe.Nikaanza kuona naanza kumudu maisha, napata hela ya kuweka na kula na watoto wangu.
Amesema kabla ya kuingia kwenye Mfuko wa Maendeleo ya tasaf maisha yake yalikuwa magumu hadi ilifikia hatua ya kukata tamaa kabisa hali iliyokuwa inamfanya kufikiria mambo mengi sana lakini baada ya kupata uwezeshwaji na Mafunzo kupitia Kwa waratibu wa Tasaf Manispaa ya Moshi na kuazia kufanya shughuguli za Ufugaji maisha yaliaza kubadilika .
"Kupitia fedha za TASAF nikaanza kufuga ng'ombe,kuku,baya na baadae sungura.Nina uhakika wa chakula na mahitaji mengine.Nasomesha watoto wangu wawili Chuo Kikuu .Kwakweli nawashukuru sana TASAF kwani wamebadilisha maisha yangu.Niko tayari kuondolewa kwenye mpango maana wako wengine wenye uhitaji."
Wakati huo huo Sarah Shengwatu ambaye ni fundi cherehani na Mkazi wa Mtaa wa Kilimani katika Kata ya mkazi wa mtaa wa kaliman ,kata ya karoleni naye ni mnufaika wa TASAF ambapo akizungumza na waandishi wa habari amesema kwakifupi mambo yake yalikuwa magumu sana na ilifika wakati alikuwa anakula hadi mlo mmoja Kwa siku akibahatika miwili lakini Sasa mambo yake yanakwenda vizuri .
Amesema awali shughuli zake za kushona alikuwa anafanyia nyumbani lakini kutokana na kunufaika na TASAF hivi sasa amefungua ofisi yake ya ushonaji na anamudu kulipa Kodi.
Hata hivyo wakati wanuifa hao wakionesha utayari wa kuondoka katika Mfuko huo tayari iko kwenye tathmini ya mwisho ya awamu ya pili ya mpango wa tatu wa kuwezesha kaya maskini nchini kuhakiki wafaidikaji wa mfuko huko ambao hali zao za maisha zimeimarika kutoka katika hali ya awali ya ufukara ili kuziondoa na kuingiza kaya zingine.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Shedrack Mziray hadi kufikia Septemba 2024 kaya 400,000 zitaondolewa na kuanza mchakato wa kuingiza kaya mpya zenye hali duni ya maisha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...