CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam kwa kushirikiana Chuo kikuu Cha Zhejiang kutoka China wamefungua Mkutano wa Pili unawakutanisha wataalamu wa elimu kada ya sayansi kwa lengo la kuwasaidia wataalamu hao kutambua namna bora ya ufundishaji wa masomo ya sayansi.
Aidha Prof. Msoffe ameeleza kuwa nchi ipo katika maboresho makubwa ya mtaala wa elimu ambao unasisitiza elimu ya sayansi, suala la Hisabati, utafiti pamoja na ubunifu.
"Ukiangalia kwa makini mtaala wetu mpya unamtaka Mwanafunzi au yule anaejifunza aweze kupambana na yyanayotokea sasa au yaale yajayo,maana yake ni kwamba tunamtengeneza tunamtengeneza Mwanafunzi atakayetumika hapa Tanzania aau katika dunia"ameeleza.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema kuwa mkutano huo umefanyika kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanywa ambapo watafiti nchini watapata wasaa wa kueleza matokeo ya tafiti zao jinsi zinavyoweza kuisaidia jamii.
Naye Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu Cha Zhejiang amesema urafiki kati ya China na Tanzania unatoa nafasi ya kubadilishana walimu wa masomo ya sayansi ambapo yataleta tija kwa maendeleo ya dijitali na kuchagiza ongezeko la wasomi wa kidijitali.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu,Prof .Peter Msoffe wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jana 11,2024 katika Ukumbi wa UDSM Jijini Dar es Salaam.
"Ukiangalia kwa makini mtaala wetu mpya unamtaka Mwanafunzi au yule anaejifunza aweze kupambana na yyanayotokea sasa au yaale yajayo,maana yake ni kwamba tunamtengeneza tunamtengeneza Mwanafunzi atakayetumika hapa Tanzania aau katika dunia"ameeleza.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema kuwa mkutano huo umefanyika kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanywa ambapo watafiti nchini watapata wasaa wa kueleza matokeo ya tafiti zao jinsi zinavyoweza kuisaidia jamii.
Naye Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu Cha Zhejiang amesema urafiki kati ya China na Tanzania unatoa nafasi ya kubadilishana walimu wa masomo ya sayansi ambapo yataleta tija kwa maendeleo ya dijitali na kuchagiza ongezeko la wasomi wa kidijitali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...