CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam - UDSM kupitia Shule Kuu ya Biashara kwa kushirikiana Benki ya Taifa ya biashara NBC imeendesha mafunzo kwa wakinamama katika masuala ya uongozi na kuweka mikakati ya kibiashara, masoko, rasilimali watu, uhasibu na mazingira ya biashara ili kuwaongezea uwezo na ufanisi wenye tija kwenye ukuaji wa maendeleo ya biashara zao na kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini.

Mafunzo hayo yamekuja kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuwa na mbinu bora ya uongozi na usimamizi mzuri wa biashara ambapo Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 za biashara zote mpya zinazoanzishwa kila mwaka zinakufa kutokana na uongozi mbovu na usimamizi usio ridhisha, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kutokuwa miongoni mwa wanawake ambao biashara zao zinakufa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Julai 5, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo hayo kwa wakinamama takribani 130, Mwakilishi wa Mtendaji wa NBC Anne Mwasika amesema mafunzo hayo yamewajengea wakinamama kuwa na ubunifu katika biashara, ubunifu wa mbinu za mauzo, ubunifu wa bidhaa na huduma bora na kuwajengea tabia sahihi ya utunzaji wa kumbukumbu na ufuatiliaji wa fursa mbalimbali ambazo zitawasaidia kuboresha biashara.

“Mafunzo kwa wakinamama yanalenga katika mambo makubwa manne yaani masuala ya uongozi na kuweka mikakati ya kibiashara, masoko na rasilimali watu, uhasibu na mazingira ya biashara ili kuwaongezea uwezo na ufanisi wenye tija kwenye ukuaji wa maendeleo ya biashara zao na kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi” amesema Mwasika

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Utafiti (UDSM) Prof. Nelson Boniface amesema wanatoa fursa kwa wakinamama kupitia wiki ya utafiti na ubunifu ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka hapo chuoni, itawapa fursa ya kuonyesha bidhaa zao na kuwaongeza kwenye madawati yao ili waweze kuonyesha bidhaa katika maonyesha ya Sabasaba ambayo yanawashiriki wengi jambo ambalo litawasaidia kukuza bunifu na biashara zao ili ziweze kuleta manufaa na tija kwa jamii.

Aidha, Prof. Boniface amesema wamefungua milango kwa wakinamama wote ambao wanafanya bunifu mbalimbali kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kutoa fursa kutoka kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakifanya bunifu kuweza kuzitumia kama sehemu ya kuzitangaza na kuleta manufaa na faida kwa wanafunzi, chuo na wafanyabiashara kwa ujumla.

Naye Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Goodluck Urassa amesema mafunzo hayo yameendelea kuwa na mwitikio mkubwa kwa wakinamama na wameonekana wanaweza kwa kuwa wanabiashara ambazo zinaweza kukua na niwapambanaji wakubwa na huwa wanashirikisha jamii kwa kutoa elimu wanayoipata kwa watoto wao na wakinababa hivyo tutaendelea kutoa kipaumbele kwao.
Mwakilishi wa Mtendaji wa NBC Anne Mwasika akizungumza Julai 5, 2024 wakati wa kufunga mafunzo kwa wakinamama katika masuala ya uongozi na kuweka mikakati ya kibiashara, masoko, rasilimali watu, uhasibu na mazingira ya biashara ili kuwaongezea uwezo na ufanisi wenye tija kwenye ukuaji wa maendeleo ya biashara zao na kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Utafiti (UDSM) Prof. Nelson Boniface akizungumza Julai 5, 2024 wakati wa kufunga mafunzo kwa wakinamama katika masuala ya uongozi na kuweka mikakati ya kibiashara, masoko, rasilimali watu, uhasibu na mazingira ya biashara ili kuwaongezea uwezo na ufanisi wenye tija kwenye ukuaji wa maendeleo ya biashara zao na kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Goodluck Urassa akizungumza Julai 5, 2024 wakati wa kufunga mafunzo kwa wakinamama katika masuala ya uongozi na kuweka mikakati ya kibiashara, masoko, rasilimali watu, uhasibu na mazingira ya biashara ili kuwaongezea uwezo na ufanisi wenye tija kwenye ukuaji wa maendeleo ya biashara zao na kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.


Washiriki wa mafunzo wa mafunzo wakiwa katika hafla ya kufunga mafunzo ya masuala ya uongozi na kuweka mikakati ya kibiashara, masoko, rasilimali watu, uhasibu na mazingira ya biashara ili kuwaongezea uwezo na ufanisi wenye tija kwenye ukuaji wa maendeleo ya biashara zao na kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini ambapo mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...