NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) ikiongozwa na mwenyekiti wake Taifa Shekh Alhad Mussa Salum wametembelea banda la Kampuni ya Superdoll Tanzania kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara kimataifa Dar es salaam SABABASA, kujionea bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na kusambazwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na katika Maonesho hayo jana Julai 2, 2024, ,Meneja wa Maendeleo ya Biashara Superdoll Bw.Adam Lubago amewakaribishwa wananchi wote kutembelea banda lao kujifunza na kujionea bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

Amesema bidhaa za kampuni hiyo ni  imara na zinadumu kwa muda mrefu ambapo miongoni mwa bidhaa hizoo ni pamoja na bidhaa za kisasa za kubeba mizigo ambazo hazitoi hewa ukaa na vilevile kampuni hiyo inatambulika kwa kuzalisha trela madhubuti zinazodumu kwa muda mrefu.

"Mpaka leo hii unaweza kukutana na trela ambazo tulizitengeneza zaidi ya miaka 25 bado ziko barabarani, utakuta zimeandikwa doll au superdoll"amesema.

Aidha Bw.Lubago ameeleza kuwa wanauza spea za magari,vifaa vya gereji,vifaa vya kubeba mizigo mikubwa, sambamba na Jenereta kubwa zisizotoa sauti ambapo zinajiendesha kiotomatiki.

Pamoja na hayo Lubago amesema wanatoa huduma ya mataili mbalimbali kutoka kampuni tofauti tofauti ambapo amebainisha kuwa yapo kwa ajili ya magari ya migodini,magari madogo pamoja na makubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...