NA FARIDA MANGUBE

Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo   kinatarajia kuanzisha kituo wezeshi cha kuwawezesha wataalamu mbalimbali wa kilimo kutoka China kuja kutoa elimu ya teknolojia mbalimbali za kilimo, mifugo na uvuvi hapa nchini zitakazowawezesha watanzania kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara ya wanafunzi  kutoka Chuo Kikuu cha  Kilimo China (CAU),  kutembelea maeneo mbalimbali ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)   kwa lengo la kujifunza,  Mkurugenzi katika Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhauwilishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalamu SUA,  Prof. Japhet Kashaigili    amesema,  lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiana upande wa wataalamu wa kilimo kutoka nchini China.

Aidha Prof. Kashaigili amesema kuwa kupitia mahusiano haya wanatarajia kupata teknolojia itakayomwezesha mkulima kulima kilimo chenye tija pia yatawezesha kujenga kituo wezeshi cha kilimo ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo   kwa ajili ya kuendesha makongamano kwa wataalam kutoka China, kuja kuonesha utaalamu mbalimbali kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.

“Kituo hiki kitawezesha vijana kupata utaalamu wa kutosha kuhusu kilimo, na mahusiano haya tuliyoyaanza yaweze kuwa na tija na yawe endelevu na paia kituo hicho kitakuwa na maabara mbalimbali  za uzalishaji na teknologia zitakuwepo za kutoka China tena wezeshi,  zitakuwa za kibiashara ambapo China na Tanzania zitapata faida kupitia kituo hicho. Leo  tumepokea wanafunzi kutoka china na walimu wao kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujifunza alisema Prof.  Kashaigili”.










 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...