Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Khamis Abdulla ametoa Rai kwa Wanufaika wa ufadhili wa Mafunzo ya muda mrefu awamu ya pili kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali wanaokwenda kusoma Ughaibuni kuwa maarifa na ujuzi wakaopata huko usaidie kuunga si taaluma zao tu bali kuwa mabalozi kwa Watumishi wenzao na Mustakabali mzima wa kubuni,kueleimisha na kusukuma gurudumu la mabadiliko ya Kidijitali hapa Nchini.

Katibu Mkuu huyo amesema hayo leo July 12,2024 Jijini Dodoma katika hafla ya kutoa vyeti na kutia saini Mkataba wa kutumikia Serikali baada ya kumaliza Masomo kwa Watalaam wa Tehama waliopata ufadhili kupitia kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Na kuongeza kuwa wao kama Wizara wamekamilisha masuala mbalimbali na kuendelea kuyafanya baadhi mfano kukamilisha mkakati wa miaka 10 wa uchumi wa Kidijitali ambapo umelenga ujuzi wa jamii ya Kidijitali.

"Hivyo ninatoa rai kuwa maarifa na ujuzi mtakaopata utusaidie kuunga sio tu taaluma zenu bali kuwa mabalozi kwa Watumishi wenzenu kwa mustakabali mzima wa kubuni,kuelimisha na kusukuma gurudumu la mabadiliko ya Kidijitali hapa Nchini hasa katika Teknolojia zinazoibukia".

"Sisi kama Wizara tumekamilisha baadhi ya masuala mbalimbali tunaendelea kuyafanya mfano, tumekamilisha mkakati wa miaka 10 wa uchumi wa Kidijitali, mkakati umekamilika ambapo pamoja na masula mengine mkakati umelenga ujuzi wa jamii ya Kidijitali ambayo ni kuwa na jamii inayojua hii Teknolojia katika biashara na mambo mengine ya biashara mtandao".

Naye Salvatory Mbilinyi Mkurugenzi Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ameewaasa wanufaika hao kutokubeza tamaduni za watu pale watakapokwenda masomoni hasa tamaduni za mavazi japo inategema na nchini husika,ili kutojiingiza katika malumbano yasiyo ya lazima.

"Sisi Watanzania tuna tamaduni tofauti na wenzetu msiende kubeza tamaduni za watu,mfano katika mavazi maana unaweza kukutana na mtu kavaa ambavyo huwezi kuelewa usioneshe kuchukizwa na Utamaduni wake,we muangalie kama alivyo kwasababu anaweza kuchukia pia,lakini hiyo inategemea umeenda nchi gani".

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi na utawala bora Ibrahim Mahumi amewataka wakafuate Sheria,Taratibu na Kanuni na kuongeza kuwa ni mategemeo ya Ofisi ya Raisi na Utumishi na Serikali kwa ujumla kuwa wanufaika hao watakapo kwenda masomoni watafanya kile ambacho kinakusudiwa kufanyika na sio Mambo mengine.

"Kwahiyo ni mategemeo ya Serikali na Ofisi ya Raisi Utumishi na utawala bora kama ndio muajiri Mkuu kwamba mtakapokwenda huko mtafanya kile kilichokusudiwa kufanyika kufanyika na vinginevyo,. Mundane mkafate Sheria,Taratibu na Kanuni ".

Akitoa Shukurani kwa niaba ya wanufaika wote Mhandisi Mwandamizi kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote Brian Kasuma amesema kuwa watatumia fursa hii adhimu kwa kujibiidisha katika masomo ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi na hasa katika uchumi wa Kidijitali na kuahidi kuwa mabalozi wa kuitangaza Tanna vivutuo vyake.

"Tunaahidi kutumikia vyema fursa hii adhimu kwa kujibidiisha katika masomo ili kuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu hasa katika uchumi wa Kidijitali. Pia tunaahidi kuwa wazalenndo wa nchi yetu na mabalozi wazuri wa jamii ya nchi yetu kwa kutii sheria na taratibu nchi husika tunazoenda kusoma na kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii kila tutakapopata nafasi".

Idadi ya Wanufaika waliosaini Mkataba na kupokea vyeti kwa siku ya leo hapa Jijini Dodoma ni 30 ambapo ni awamu ya pili na awamu ya kwanza walikuwa 20 hivyo jumla wamefikia 50 ambapo ndio idadi iliyokuwa ikihitajika.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...