Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya na Mjumbe Maalum wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 11.07. 2024 amewasilisha ujumbe maalum wa Mhe. Rais Samia kwa Mhe. Mohamed Ould Ghazouani, Rais wa Jamhuri ya Mauritania.


Ujumbe wa Rais Samia umepokelewa na Mhe. Mohamed Bilal, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mauritania.

Mhe. Bilal baada ya kupokea ujumbe huo maalum kwa niaba ya Rais Ghazouani alisema kuwa, atamfikishia ujumbe huu maalum Mhe. Rais na amezipongeza nchi mbili hizi kwa ushirikiano wa kidugu uliodumu kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Mhe. Ummy Mwalimu ameipongeza Serikali ya Mauritania kwa mapokezi mazuri ambayo wameipatia timu ya ujumbe maalum wa Dkt.Samia na ameahidi kuendeleza mashirikiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...