Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa Jimbo la Misungwi , leo Agosti 14, 2024, mara baada ya kuwasili na kupokelewa Mkoa wa Mwanza, kuanza ziara ya siku 2 ya kikazi mkoani humo, akitokea Mkoa wa Geita.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Malengo ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2024, kukagua na kuhamasisha uhai wa CCM, pamoja na kuzungumza na kuwasikiliza wananchi








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...