IMEELEZWA kuwa zaidi ya shilingi bilioni 43 zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Viti Maalum Kundi la Wenye Ulemavu na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tarafa ya Lyamungo mara baada ya kutembelea Tarafa ya Machame na Masama.

Nderiananga alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuchochea maendeleo ya Jimbo na Hai na akatumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la MpigaKura ili kuwa na haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025.

“Tunaenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu wakati ukifika mjitokeze mjiandikishe pamoja na daftari la mkaazi sasa kupitia uchaguzi huu wa serikali za mitaa kama tunaona wanawake wanakubalika katika maeneo yao wapewe fomu wagombee bila upendeleo kwa kuzingatia uwezo wao wa kazi,” Alisema Nderiananga.

Aidha aliendelea kuwaomba wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule wakiwemo wenye ulemavu ikiwa ni haki yao kisheria ya kupata elimu badala ya kuwafungia ndani na kuwafanyia vitendo vya kikatili ambavyo huwaathiri kisaikolojia na kuharibu ndoto zao.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...