Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka Mamlaka za serikali pamoja na wawekezeji kutoka sekta binafsi kutumia fursa zilizopo katika sheria ya PPP kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuipunguzia serikali mzigo wa kibajeti.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 31 ,2024 jijini Dodoma katika Mkutano wa mafunzo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na Matumizi sahihi ya Takwimu kwa Wakuu wa Mikoa ,Makatibu Tawala wa Mikoa ,Wakuu wa Wilaya ,Wakurugenzi wa Halmashauri,Waganga wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya.

Pia Dkt. Nchema amewaagiza Maafisa Masuuli wote nchini kuzingatia maelekezo ya waraka wa Hazina namba 7 wa mwaka 2020 -2021 unaotoa maelezo na muongozo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa utaratibu wa PPP

“Taifa lolote ulimwenguni ni matumizi sahihi ya Takwimu zilizozalishwa na vyombo vyenye jukumu hilo kwa mnaofahamu maendeleo yeyote ya nchi yatafanyika kwa mafanikio endapo Takwimu sahihi zitatumika,” amesema

Hata hivyo Dkt.Nchemba amesema eneo muhimu lililowekwa katika sheria ya ununuzi wa umma kwa makusudi ya kuwainua watanzania ni ushiriki wa kampuni za Kitanzania katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, ambapo katika hilo kampuni za kitanzanaia ndizo zitakazopaswa kuwa kampuni kiongozi ambazo ndizo zitakazokuwa na jukumu la kutafuta kampuni nyingine itakayoshirikiana nazo katika utekelezaji wa mradi husika ,ikiwemo kusimamia thamani ya fedha.

Aidha ametoa wito kwa watanzania kujenga tabia ya kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuendelea kukuza uchumi wa ndani ya nchi.

“Kumekuwa na wimbi la watanzania kuamini kuwa bidhaa kutoka nje ndio imara na kuacha kutumia bidhaa za ndani yaani unakuta mtanzania anakwenda kufungua kiwanda nje ya nchi ili aingize tu bidhaa kutoka nje wakati anaweza kufungua kiwanda hicho ndani ya nchi na kuzalisha hapahapa nchini ili kujenga uchumi wa ndani,” ameeleza Nchemba

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt . Festo Dugange ameelezea changamoto zilizojitokeza baada ya kuanza kutumia mfumo mpya wa manunuzi wa (NeST) hasa katika utekelezaji wa miradi inayotumia FORCE ACCOUNT
Ambapo amesema kutokana na Mfumo huo umesababisha kasi kupungua ila katika mafunzo hayo anaamini kuwa elimu itakayotolewa itasaidia kutoa jibu sahihi ili kusaidia utekelezaji wa miradi bila kusuasua.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...